Home LOCAL MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU MADALE, WAJADILI CHANGAMOTO NA MAFANIKIO

MKUTANO MKUU WA MWAKA WA WADAU MADALE, WAJADILI CHANGAMOTO NA MAFANIKIO

Stephen Kazimoto Mwenyekiti wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam.

…………………….

Kikundi cha Wadau Madale Group wamekutana na kufanya mkutano mkuu wa Mwaka eo  kwenye ukumbi wa  Lemoon Garden Madale ikiwa ni kujadili maendeleo pamoja na changamoto mbalimbali zinazokabili kundi hilo.

Kikundi cha Wadau Madale kina takribani miaka mitano(5) ambapo wadau hao wamekuwa wakisaidiana kwenye mambo mbalimbali ya kijamii.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Wadau Madale Group Bw.Stephen Kazimoto wakati akizungumza na Wanachama Katika mkutano wa Mwaka wa kikundi hicho uliofanyika Leo jijini Dar es Salaam na kushirikisha wanakikundi.

Moja wapo ya baadhi ya Vipengele ambavyo vipo kwenye katiba ya Wadau Madale Group  ni kuwepo kwa michango ya msiba endapo mmoja wa wadau atapata msiba, kuwepo kwa ulazima wa michango ya mkutano mkuu kwa kila mdau ambapo mkutano huo utafanyika kila mwaka, matangazo ya Biashara kwa kila meza ni shilingi elfu ishirini (20) hii kwa ajili ya wajasiriamali wadogo wadogo.

Aidha mkutano wa leo tarehe 10 Decemba 2022 umeazimia kutokuwepo kwa uchaguzi wowote wa viongozi hivyo viongozi wa zamani wataendelea kushikilia nafasi zao kwa kipindi cha miaka mitatu (3), kuwepo kwa ada ya elfu ishirini(20) kila mwezi kwa kila mdau ambapo mchango huo utakuwa na Kwa ajili ya kuchangia Wadau pindi wanapopata misiba ya wao wenyewe au wategemezi.

Ifikapo mwaka 2023 kikundi cha wadau kitakuwa tayari kishafungua akaunti ambapo michango yote itakuwa inawekwa kwenye akaunti hiyo lakini pia wadau watafungua Sacoss na wanakaribisha wadau ambao watapenda kujiunga

wadau wameshauri kuwepo kwa jumbe za simu za kawaida ambazo sikitumwa zinaweza mfikia mdau yeyote hata kama anatumia simu isiyokuwa na WhatsApp.

Hata hivyo viongozi wa Wadau mlMadale Group  wameendelea kutoa shukurani kwa wadau wa Madale kushiriki vyema katika mambo mbali mbali ya kijamii lakini pia amewaomba baadhi ya wadau wasiokuwa waaminifu kubadilika na kutoa michango kwa wakati ili waweze kufanikisha kikundi hicho kufika mbali na kufanikisha malengo kwa wakati.

Elesia Mbuya Katibu wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam

Mmoja wa Wanachama wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam

Frank Magige Mhazini wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam

Gration Mbelwa Mwenyekiti mstaafu Wadau Madale wa Wadau Madale akizungumza kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam

Picha mbalimbali zikiwaonesha Wanachama wa Wadau Madale wakiwa kwenye mkutano mkuu wa Mwaka wa Wadau hao Leo uliofanyika kwenye ukumbi wa Lemoon Catering mkabala na Kituo Cha Polisi Madale Kata ya wazo wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam

Previous articleNCHI IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA UJENZI WA MAENDELEO – WAZIRI SIMBACHAWENE
Next articleWAFANYABIASHARA WILAYA YA CHATO WATAKIWA KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA BIASHARA ZAO.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here