Home BUSINESS MFUMO WA UMILIKISHWAJI FUKWE KUPITIWA UPYA ILI KURAHISISHA UWEKEZAJI WA MAENEO YA...

MFUMO WA UMILIKISHWAJI FUKWE KUPITIWA UPYA ILI KURAHISISHA UWEKEZAJI WA MAENEO YA FUKWE

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Wizara ya Maliasili na Utalii imependekeza kupitiwa upya kwa mfumo wa umilikishwaji wa fukwe ili kurahisisha mazingira ya uwekezaji na usimamizi wa maeneo ya fukwe nchini kwa lengo la kukuza utalii wa fukwe.

Ameyasema hayo leo jijini Mwanza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la Nane la Maendeleo endelevu lenye dhima ya usimamizi madhubuti wa fukwe kwa maendeleo endelevu.

“Tunapendekeza mfumo wa umilikishwaji fukwe upitiwe upya ili ikiwezekana umiliki uhamishiwe katika wizara mojawapo kama Wizara ya Uwekezaji au Sekta ya Utalii kurahisisha uwekezaji na kutengeneza mazingira bora zaidi ya fukwe hizo” Mhe. Masanja amesisitiza.

Amefafanua kuwa pendekezo hilo linatokana na maoni ya kikosi kazi kilichoundwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kilichopitia fukwe hizo na kugundua kuwa asilimia kubwa ya fukwe zinamilikiwa na watu binafsi lakini nyingine zinamilikiwa na Serikali za mitaa, hivyo kupelekea kutokuwa na uelewa wa pamoja juu ya uwekezaji katika maeneo ya fukwe.

Amesema changamoto hiyo inaweza kutatuliwa kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi ili kuweka uelewa wa pamoja juu ya uwekezaji katika maeneo ya fukwe na kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji kuweza kuzifikia fukwe hizo kwa urahisi.

Aidha, amesema kikosi kazi hicho kilichoundwa mwaka 2016 kilitembelea mikoa kadhaa ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Tanga ,Mtwara na Lindi kwa lengo la kuzitambua na kuziainisha fukwe zilizopo katika maeneo hayo na hatimaye kuleta mapendekezo ya kuzitambua fukwe na kuangalia umiliki wake sambamba na kuangalia jiografia zinazofaa kama zinawiana na masuala ya utalii.

Previous article ZIARA YA MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN WILAYANI MONDULI
Next articleKAIMU MKUU WA MKOA WA MWANZA ATEMBELE BANDA LA BoT WIKI YA HUDUMA ZA FEDHA MWANZA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here