Home LOCAL UMMY MWALIMU HAPOI, AENDELEA KUWAOMBEA KURA WAGOMBEA WA CCM UCHAGUZI S/MITAA.

UMMY MWALIMU HAPOI, AENDELEA KUWAOMBEA KURA WAGOMBEA WA CCM UCHAGUZI S/MITAA.

Na: Mwandishi Wetu, Tanga.

Novemba 22, 2024, Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ummy Mwalimu ameingiza katika siku ya pili kuwanadi wagombea wa nafasi za uenyeviti wa mitaa katika mitaa minne ya Jimbo la Tanga Mjini.

Katika mikutano minne aliyoshiriki, Ummy Mwalimu amewaombea kura wagombea wa mitaa ya Suji (Kata ya Mzingani), Gofu Juu (Kata ya Nguvumali), Kasera (Kata ya Maweni) na Chumvini (Kata ya Chumbageni), ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza kuwa wagombea watokanao na CCM ndiyo wagombea bora wenye uwezo na weledi wa kutatua shida za wananchi, Hivyo wananchi wasifanye makosa, wawachague wagombea wa CCM ili kutatuliwa kero zao na kuharakisha maendeleo ya mitaa yao.

“Ndugu zangu, niwasihi, tuwachague wagombea wa CCM, Hawa ndiyo wenye uwezo wa kutatua kero zenu. Siku ya kupiga kura hakikisha unachagua Mwenyekiti na Wajumbe kutoka CCM, Kwa kufanya Hivyo, utakuwa umechagua maendeleo.” amesisitiza Ummy Mwalimu.

Sanjari na hilo, Ummy Mwalimu amesema mitaa na kata zote za Jimbo la Tanga Mjini zimepiga hatua kubwa za kimaendeleo hasa katika uboreshwaji wa huduma za kijamii kama vile elimu, afya, maji, miundombimu ya barabara kutokana na kazi nzuri zinazofanywa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kuipatia Tanga Mjini fedha nyingi za kugharamia na kutekelezaji miradi ya maendeleo.

Aidha, amewaeleza wananchi hao kuwa fedha nyingi zimeletwa kuhakikisha miradi ya zamani na mipya inatekelezwa, kwahiyo wananchi wana kila sababu kuwaamini wagombea wa CCM kwani kiu ya CCM ni kuwaleta wananchi maendeleo.

Ummy Mwalimu amesisitiza pia kuwa yupo bega kwa bega na wagombea wote wa nafasi za uenyeviti wa mitaa pamoja na wajumbe wao ili kuhakikisha CCM inaibuka mshindi na kuongoza mitaa yote 181 ya Jimbo la Tanga Mjini.

Katika hatua nyingine, wagombea hao wa mitaa minne, wamewaomba wananchi wawachague kwani wanajua shida za wananchi na wamejipanga kuzitatua shida zote kwa ushirikiano na viongozi wengine wa chama na serikali.

Previous articleMITAALA IZINGATIE MABADILIKO YA KIUCHUMI NA TEKNOLOJI-MAJALIWA
Next articleUMMY MWALIMU AANZA KWA KISHINDO KUWANADI WAGOMBEA WA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA TANGA MJINI.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here