Na: Mwandishi Wetu
Tanzania yashiriki mkutano wa kidiplomasia wa ukamilishwaji wa sheria ya kimataifa ya Miliki Ubunifu katika Rasilimali za Kijenetiki na Maarifa ya Jadi yanayohusiana na Rasilimali za Kijenekiti unaofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) kuanzia tarehe 13 Mei, 2024 hadi 24 Mei, 2024 jijini Geneva, Uswisi
Sheria hiyo ya Kimataifa inalenga kuhakikisha mfumo wa ulinzi wa Miliki Ubunifu unatambua matumizi ya Rasilimali za Kijenetiki na Maarifa ya Jadi ili kuwanufaisha wamiliki wa rasilimali hizo
Ujumbe kutoka Tanzania unaongozwa na Mheshimiwa Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na Mashirika ya Kimataifa Dkt Abdallah Possi akiambatana na Afisa Mtendaji Mkuu kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) Bw. Khamis Juma Khamis, Msajili wa Hakimiliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu za Mimea Wizara ya Kilimo Bw. Twalib Njohole, na Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu kutoka BRELA Bi. Loy Mhando.