Home LOCAL PPAA YAJIPANGA KUWANOA WAZABUNI, TAASISI NUNUZI JUU YA MFUMO MPYA WA KUWASILISHA...

PPAA YAJIPANGA KUWANOA WAZABUNI, TAASISI NUNUZI JUU YA MFUMO MPYA WA KUWASILISHA RUFAA KIELETRONIKI

Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando akielezea moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika kipindi cha Power Breafast cha Clouds FM, Jijini Dar es Salaam

Ili kukabiliana na mageuzi yaliyofanyika katika Sheria mpya ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA) imejipanga kutoa mafunzo ya mfumo mpya wa kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na Rufaa kwa njia ya kieletroniki (Complaint and Appeal Management) kwa wazabuni na taasisi nunuzi wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Pwani.

Katibu Mtendaji wa PPAA, Bw. James Sando amewasihi wazabuni na taasisi nunuzi wa mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro, Tanga na Pwani kuhakikisha wanashiriki mafunzo hayo muhimu ili kuwajengea uwezo wa kujua jinsi kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kielektroniki pindi wanapoona hawakutendewa haki katika michakato ya ununuzi.

Bw. Sando ametoa wito huo leo tarehe 10 Mei 2024, alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha “Power Breakfast” cha Clouds Fm Jijini Dar es Salaam juu ya Moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki katika Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (NeST) uliojengwa chini ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Kutokana na mabadiliko ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023, ambayo inazitaka taasisi nunuzi na wazabuni kutumia (NeST), PPAA kwa kushirikiana na PPRA tumejenga moduli mpya ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kwa njia ya kielektroniki ili kukidhi matakwa ya sheria” amesema Bw. Sando

Bw. Sando ameongeza kuwa kuanzishwa kwa moduli ya kuwasilisha na kushughulikia malalamiko na rufaa kielektroniki (Complaints and Appeals Management) katika Mfumo wa NeST, PPAA itaweza kufanya mapitio ya mchakato mzima wa zabuni inayolalamikiwa na kuiwezesha Mamlaka Rufani kupata uhalisia zaidi na kutoa uamuzi kwa wakati, haki na usawa.

Bw. Sando aliongeza kuwa, Sheria ya ununuzi wa umma imekuwa ikifanyiwa maboresho kila baada ya kipindi fulani kutokana na mahitaji pamoja na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.

Previous articleMATUKIO KATIKA PICHA: WAZIRI MKUU AKIWA BUNGENI
Next articleWAZIRI MKUU MGENI RASMI TULIA MARATHON
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here