Home BUSINESS MAMIA YA WAFANYAKAZI KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED WASHIRIKI MEI MOSI...

MAMIA YA WAFANYAKAZI KAMPUNI YA MATI SUPER BRANDS LIMITED WASHIRIKI MEI MOSI MANYARA .

 

Ferdinand Shayo ,Manyara .
 
Mamia ya Wafanyakazi wa Kampuni ya kuzalisha vinywaji changamshi ya Mati Super Brands Limited wameshiriki maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi ya Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa Katika Viwanja vya Tanzanite Kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara na kupambwa na msafara mrefu wa magari ya kusambaza vinywaji kutoka kwenye kampuni hiyo.
 
Mkurugenzi wa Kamapuni hiyo David Mulokozi amesema kuwa maonyesho hayo ya magari yaliyotanguliwa na farasi yanalenga kuonyesha ukubwa wa kampuni hiyo katika kusambaza bidhaa zake za Strong Dry Gin,Tanzanite Premium Vodka na Sed Pineapple flavoured gin.
Mulokozi amesema kuwa kampuni hiyo itaendelea kuwahakikishia wafanyakazi wake Maslahi bora ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi.
 
Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wafanya kazi ili waweze kutimiza majukumu yao na kuleta tija mahali pa kazi.
 
Twange amepongeza serikali pamoja na sekta binafsi kwa kuwa mstari wa mbele kuajiri na kupunguza changamoto ya ajira nchini.
Previous articleSERIKALI YA Dkt. SAMIA IMEENDELEA KUSIMAMIA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI – Prof. BUSAGALA 
Next articleHUAWEI CALLS ON DEVELOPERS TO BUILD NATIVE APPS FOR HARMONYOS
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here