Home BUSINESS WATALII WANASEMA KULALA BEI CHEE MIKUMI TOFAUTI NA MAENEO MENGINE

WATALII WANASEMA KULALA BEI CHEE MIKUMI TOFAUTI NA MAENEO MENGINE

*Kwa buku tano tu unalala hifadhini

*Msosi unaanzia shilingi elfu moja mia tano

*Waliokuwa wanaogopa kuhofia gharama kubwa watolewa hofu, wakaribishwa

Watanzania wanaotaka kwenda kutalii hifadhini na kusita kufanya hivyo wakihofia gharama kubwa za kulala hotelini wawapo hifadhini wametolewa hofu hiyo kutokana kuwepo kwa malazi mazuri yanayomilikiwa na TANAPA ambayo bei zake ni nafuu

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wanahabari waliotembelea hifadhi ya Taifa mikumi mhifadhi mkuu wa hifadhi hiyo Kamishina Msaidizi wa Uhifadhi Agustine Masesa na Mhifadhi Msaidizi Herman Mtei wamewataka watanzania wakafurahie maisha hifadhini bila hofu ya gharama

“Kama mlivyoona hapa tuna vyumba vinavyoanzia shilingi elfu tano, tunavyo pia vya elfu 23 kwa mtu mmoja ambayo hii unapata na chai ya asubuhi kizungu wanaita breakfast”- amesema Masesa

Masesa ameongeza kuwa hata gharama za vyakula ukiwa hifadhini humo ni nafuu sana kwani vyakula vinaanzia shilingi elfu moja mia tano

“Ukiwa na buku jero unafika sehemu ya kulia chakula na unapata msosi bila shida yoyote, lazima watanzania wajue kuwa gharama sio kubwa kabisa na inawezekana kuja kufurahia maisha ” ameongeza Masesa

Kwa upande wake Mtei amesisitiza kwa wanaopenda vinywaji vya kileo na laini kuwa bei ni ile ile waliyoizoea mtaani na kuongeza kuwa kuna baadhi ya maeneo mtaani bei za vinywaji huwa ghali kulinganisha na hifadhini

“hapa bei ya vinywaji ni nafuu sana, unapata bia kwa elfu mbili tu kama uko nje, soda elfu moja na hata maji unanunua kwa gharama za kawaida “- amesisitiza Mtei

Kwa kipindi kirefu dhama imejengeka kuwa ni gharama kubwa kulala katika hifadhi za Taifa na hivyo kuwafanya watu kutamani kwenda kutembelea hifadhi hizo lakini wanaogopa gharama

Kufahamika kwa gharama hizi kwa wananchi kutasaidia kuimarisha na kuongeza idadi ya watalii wa ndani wanaotembelea vivutio mbalimbali vilivtopo nchini.

Previous articleWABUNGE WA AFRIKA MASHABIKI WARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI BANDARI YA DSM
Next articleRAIS DKT. SAMIA AMPOKEA RAIS DUDA WA POLAND IKULU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here