Home LOCAL WATU 3 WAFARIKI DUNIA KWA MAFURIKO MOROGORO

WATU 3 WAFARIKI DUNIA KWA MAFURIKO MOROGORO

 

Watu watatu wa familia Moja wamefariki Dunia akiwemo bibi,mama na mjukuu huku baba wa familia hiyo aliyefahamika jina la Sengo Hamis akijeruhiwa baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia january 10 na kufurika mto Mgolole Manispaa ya Morogoro

Mashuhuda wa tukio hilo amesema limetokea majira ya saa nane usiku wa kuamkia Leo January 10 mwaka huu ambapo wakati tukio linatokea nyumba ya familia hiyo ilizingirwa na maji hivyo wakati wakijiokoa kuvuka mto maji yakawazidi nguvu na kusombwa na maji

Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa Morogoro Mrakibu wa Zimamoto Shabani Marugujo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema hadi sasa wamefanikiwa kuopoa miili ya watu miwili akiwemo mjukuu aliyefahamika kwa majina ya Asnath (6)na bibi aliyefahamika kwa Thelesia Adroph anayekadiriwa kuwa na umri miaka 70 -76 huku jitihada za kuutafuta mwili wa Mwanahamis Issa bado zinaendelea.

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here