Home LOCAL UFUNGUZI WA HOSPITALI YA MKOA LUMUMBA

UFUNGUZI WA HOSPITALI YA MKOA LUMUMBA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Mjini Magharibi Lumumba Zanzibar tarehe 10 Januari, 2024.

NA Rahma Maelezo 10/01/2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Afya kuweka mpango madhubuti wa kuwasomesha madaktari kuhusu kutumia vifaa tiba ili kutoa huduma bora nchini.

Wito huo ameutoa huko Lumumba Mkoa wa Mjini Magharib katika ufunguzi wa Hospitali ya Mkoa ikiwa ni maadhimisho ya kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi.

Amesema vifaa hivyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa in vyema kuvitunza na kuvithamini ili viendelee kutoa huduma.

Aidha ameipongeza Kampuni iliyojenga pamoja na Wizara ya Afya kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kujenga hospitali hiyo kwa kuzingatia viwango vilivyotakiwa.

Aidha ameitaka Wizara kufuatilia huduma zinazotolewa kwani lengo la Mapinduzi in kuondoa unyonge wa janga la maradhi.

Katika hatua nyengine Dkt. Samia amewataka wadau na wajenzi kuhakikisha wanamaliza ujenzi huo kwa wakati ili kuimarisha afya za wananchi

Aidha amewatahadharisha wananchi kufuata taratibu wanazopewa ili kutunza miundombinu ya hospitali.

Ameongeza kuwa kabla ya Mapinduzi huduma za matibabu kwa wananchi walikuwa wakifuata masafa ya mbali hivyo kujengwa kwa hospitali za Wilaya na Mikoa Unguja na Pemba zitasaidia kuondosha usumbufu kwa wananchi wa kufuata huduma.

Akitoa taarifa ya kitaalamu Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Amour Suleiman amesema kuwa jumla ya shilingi za Kitanzania bilioni 32.5 zimetumika katika ujenzi huo kwa fedha za mkopo zinazotokana na Uviko19.

Aidha amefahamisha kuwa huduma zitakazotolewa katika hositali hiyo ni wodi ya waototo chini ya miaka 13, huduma za ICU kwa akina mama wanaojifungua pamoja na ICU kwa wagonjwa wa maradhi mbalimbali.

Ameongeza kuwa huduma nyengine zitakazotolewa pia huduma za dharura, huduma za usafishaji damu,(Analysis) huduma za Xray, Ultrasound, pua, kinywa na meno.

Mapema Waziri wa Afya Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imejenga hospitality 10 za Wilaya na moja ya Mkoa Unguja na Pemba ikiwemo Hospital ya Lumumba kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

“Tumefanikiwa kujenga hosptali 10 za Wilaya Unguja na Pemba na hospital hii moja ya Mkoa kati ya hospital hizi 10, 9 za Wilaya tayari tumeshazifungua rasmin na wananchi wanapata huduma nchi nzima” alifahamisha Waziri Mazrui.

Aidha amefahamisha kuwa katika hospitali hiyo mna Thieta 35 ikiwemo 13 za akina mama pamoja na Emagency 13 ambapo awali ilikuwepo moja katika hospitali ya Mnazimmoja.

Previous articleWATU 3 WAFARIKI DUNIA KWA MAFURIKO MOROGORO
Next articleKINANA AKUTANA NA BALOZI WA RWANDA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here