Home BUSINESS GAVANA TUTUBA ATETA NA BALOZI WA EU

GAVANA TUTUBA ATETA NA BALOZI WA EU

NA: MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania ( BoT)Emmanuel Tutuba, amekutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Christine Grau, katika Ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uchumi wetu ikiwemo kuanza kwa mfumo wa utekelezaji wa sera ya fedha unaotumia riba, ukuaji wa huduma jumuishi za fedha pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya malipo.

Katika kikao hicho, Gavana Tutuba ameuomba Umoja huo kuwajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa Benki Kuu na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya fedha na uchumi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here