Home BUSINESS TANZANIA YAANZA UENYEKITI  WA MIKUTANO YA AfCFTA

TANZANIA YAANZA UENYEKITI  WA MIKUTANO YA AfCFTA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara (STO) wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) amezisisitiza Nchi wananchama wa Mkataba huo kushirikiana kwa usawa kurekebisha sera zinazowezesha kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo.

Mwenyekiti huyo wa STO Dkt. Abdallah ameyasema hayo Januari 26, 2024 alipokuwa akifungua Mkutano wa 16 wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara wa AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia tarehe 26 hadi 29 Januari 2024 ukiongozwa na Tanzania, ambayo ni Mwenyekiti wa AfCFTA kwa mwaka huu 2024.

Akifungua Mkutano huo, Dkt. Abdallah alisisitiza kuwa Sera hizo zinazotungwa zinapaswa kuondoa vikwazo, kukuza ushirikishwaji na kuhakikisha kuwa faida za AfCFTA zinafika pembe zote za Bara la Afrika.

“AfCFTA inawakilisha ishara ya matumaini na fursa, inatufunza katika maono ya pamoja ya kukuza maendeleo endelevu kupitia biashara imara ya ndani ya Afrika.” Amesema Dkt Abdallah.

Vilevile amebainisha kuwa Kamati hiyo ina jukumu muhimu katika kuonyesha ufanisi wa utekelezaji wa malengo ya AfCFTA kwa kushiriki katika mazungumzo ya wazi yanayolenga yaliyo bora kwa Afrika kwa ujumla, badala ya nchi binafsi.

“Tunapofanya majadiliano ya kina, tuwe na mtazamo mpana wa Afrika, tukizidi nchi zetu binafsi, tukitambua kuwa kila uamuzi tunaoufanya una uwezo wa kuathiri maisha ya mamilioni ya watu. Ni jukumu letu la pamoja kuhakikisha kuwa athari hizi ni nzuri, za usawa, na endelevu”. Alisisitiza Dkt. Abdallah.

Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha (Usimamizi na Uchumi) Bw. Elijah Mwandumbya amesema Mkutanobhuo unalenga kutatua masuala ya kikodi ili kurahisisha biashara katika Bara la Afrika

Previous articleGAVANA TUTUBA ATETA NA BALOZI WA EU
Next articleLITTLE TREASURES SECONDARY YAANIKA MAFANIKIO MAKUBWA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here