Home BUSINESS GAVANA TUTUBA ATETA NA BALOZI WA EU

GAVANA TUTUBA ATETA NA BALOZI WA EU

NA: MWANDISHI WETU,DAR ES SALAAM

GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania ( BoT)Emmanuel Tutuba, amekutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Christine Grau, katika Ofisi za Benki Kuu jijini Dar es Salaam na kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uchumi wetu ikiwemo kuanza kwa mfumo wa utekelezaji wa sera ya fedha unaotumia riba, ukuaji wa huduma jumuishi za fedha pamoja na uboreshwaji wa mifumo ya malipo.

Katika kikao hicho, Gavana Tutuba ameuomba Umoja huo kuwajengea uwezo zaidi wafanyakazi wa Benki Kuu na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya fedha na uchumi ili waweze kutimiza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Previous articleAMEND TANZANIA- UBALOZI WA USWIS WATOA MAFUNZO YA USALAMA BARABARANI DODOMA
Next articleTANZANIA YAANZA UENYEKITI  WA MIKUTANO YA AfCFTA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here