Home LOCAL WANANCHI JORODOM HANANG  WAVUTIWA NA MABANGO YA UELIMISHAJI  NA DAWA ZA KUTIBU...

WANANCHI JORODOM HANANG  WAVUTIWA NA MABANGO YA UELIMISHAJI  NA DAWA ZA KUTIBU MAJI WAOMBA DAWA ZIONGEZWE  

 Na.Elimu ya Afya kwa Umma 

Kutokana na Wizara ya Afya kuweka jitihada kubwa za uelimishaji jinsi ya kujikinga na magonjwa ya mlipuko pamoja  na usambazaji wa dawa za kutibu maji katika Wilaya ya Hanang Mkoani Manyara, wananchi kutoka Kijiji cha Jorodom  wamevutiwa na jitihada hizo huku wakiomba dawa za kutibu maji ziongezwe zaidi .

Wakizungumza kijijini hapo akiwemo mwenyekiti wa Kijiji hicho wamesema hatua ya serikali kusambaza mabango ya kuelimisha kuhusu kuzingatia kanuni za afya kujikinga na magonjwa pamoja na usambazaji wa mabango ni nzuri katika kuwajali wananchi wake.

“Hii elimu ni nzuri sana maana maana inatupa mwongozo  tufanye nini  pia kitendo cha kutibu maji mnajali usalama wetu tunataka vidonge zaidi na zaidi  “amesema mmoja wa wananchi hao.

Ikumbukwe kuwa  Jorodom  ni Kijiji cha kwanza kuathiriwa na maji ya mafuriko  yaliyoambatana na maporoko ya tope ,magogo na mawe hali iliyosababisha vifo na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya maji, nyumba na vitu mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here