Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki Ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Dodoma leo tarehe 10 Desemba 2023.
Akizungumza wakati wa Ibada hiyo, Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema wakati mwingine mitandao inaumiza yamesemwa mengi na wengine Bado wanasema yeye ni mzuka,amewakumbusha waumini sehemu moja Zaburi ya 118,Aya ya 17,ambayo inasema ‘ Sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana kwa hiyo wakae na Amani yuko salama.
Amesema alikwenda nje kwa ajili ya shughuli maalum kwa takribani mwezi mmoja lakini wengine wamesema Mzee amekata moto,bado kabisa kazi ambayo Mungu amemtuma hajamaliza kuifanya