Home BUSINESS WAZIRI WA UCHUKUZI WA JAPAN KUFANYA ZIARA NA UJUMBE WA WATU 40...

WAZIRI WA UCHUKUZI WA JAPAN KUFANYA ZIARA NA UJUMBE WA WATU 40 NCHINI

Na Mwandishi wetu

Waziri wa Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii wa Japan, Konosuke Kokuba anatarajia kufanya ziara ya kikazi nchini mnamo Januari mwaka 2024.

Katika ziara hiyo, Kokuba ataongozana na ujumbe wa watu 40 kutoka kampuni binafsi zinazojihusisha na masuala ya miundombinu na baadhi ya watumishi wa Wizara yake.

Ziara hiyo imelenga kujadili fursa mbalimbali zinazotokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Japan katika maendeleo ya miundombinu.

Hayo yalijulikana Disemba 7 jijini Dar es Salaam katika kikao cha pamoja cha maandalizi ya ziara hiyo kilichoshirikisha viongozi wa Wizara ya Uchukuzi na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Plasduce Mbossa pamoja na Menejimenti yake kuongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara.

Kwa upande wa Japan, ujumbe wake uliongozwa na Yoshihiro Kakishita kutoka Sekretarieti ya Wizara ya Ardhi, Miundombinu, Uchukuzi na Utalii ya Japan.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mbosaa ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Japan kuja kuwekeza kwa upande wa miundombinu ya Bandari nchini.
Mwisho

Previous articleMAKAMU WA RAIS ASHIRIKI IBADA YA JUMAPILI,PAROKIA YA MWENYE HERI MARIA THERESA LEDOCHOWSKA
Next articleWADAU MADALE GROUP WAZINDUA SACCOS YAO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here