Home LOCAL KINANA: DIRA YA MAENDELEO ITABORESHA PATO LA MTU MMOJA MMOJA

KINANA: DIRA YA MAENDELEO ITABORESHA PATO LA MTU MMOJA MMOJA

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Komredi Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wanachama na Wananchi wa Jimbo la Chato alipowasili katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Chato mkoani Geita. Mkutano huo umehusu utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Chato kwa Mwaka 2021-2023

Na Mwandishi Wetu, Chato

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulurhaman Kinana amesema mkakati wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni kuinua pato la mtu mmoja mmoja kupitia Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Akizungumza na wananchi pamoja na wanachama wa CCM waliohudhuria mkutano mkuu wa Chama Jimbo la Chato mkoani Geita, Kinana amesema kuwa Desemba 9, 2023 Rais Samia amezindua mpango wa dira ya Taifa.

“Kwa wale ambao hamkusikiliza nitamshauri Katibu Mkuu achukue zile dondoo zilizotolewa na Waziri wa Mipango Profesa Kitila Mkumbo ampelekee kila mjumbe kwenye whatsap yake ili wajue kazi iliyofanyika. 

“Tulianza na dira ya miaka 25, iliyoanza mwaka 2000 hadi mwaka 2025 , sasa tunaandaa nyingine ya 2025/2050 ukisikiliza kwa makini ile dira ya 2020/2025 kila kitu kilichopangwa , tulichodharimia, tulichoahidi kimetekelezwa kwa zaidi ya asilimia 85.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Chato. Mkutano ulihusu utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Chato kwa Mwaka 2021-2023

“Kuanzia miradi ya maji , elimu, afya, ujasiriamali , miundombinu , umoja, amani , demokrasia , mshikamano , uwekezaji, kila jambo lililopangwa katika dira ya 2020/2025 limefanyika.Sasa tunajiandaa kwa nafasi nyingine,”amesema.

Amepongeza kuwa anaamini katika miaka 25 ijayo Serikali itaendelea kuimarisha mambo hayo yanayozungumzwa kila siku ya elimu , afya , miundombinu lakini na mkazo utawekwa katika kukuza pato la kila mtu Kwa maana ya pato binafsi.

Baadhi ya Wajumbe katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Chato mkoani Geita. Mkutano huo umehusu utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Chato kwa Mwaka 2021-2023

“Pato binafsi litakuzwa kwa kutumia mbinu na njia mbalimbali.Wakati mwingine wananchi wanalalamika, sasa mimi Kwa umri wangu nimesikiliza sana malalamiko ya wananchi, sehemu kubwa ya malalamiko yanatokana na maendeleo.

“Wananchi wakipata wamepewa maji , wanataka kitu kingine , kwa hiyo maendeleo makubwa yanafanya wakati mwingine malalamiko yawe makubwa. Nakumbuka miaka ya kwanza ya uhuru wa nchi yetu miaka ya 1970,1980 kulikuwa hamna malalamiko kwasababu maisha yalikuwa ya kawaida,”amesema.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Bara, Komredi Abdulrahman Kinana akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Chato mkoani Geita. Mkutano huo umehusu utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la Chato kwa Mwaka 2021-2023

Amefafanua wakati huo ukizungumzia barabara hazipo, maji hayapo, shule za kawaida na miundombinu ya chini,hivyo hakukua na malalamiko kwasababu huwezi kulalamika Kwa kitu ambacho hujakiona.

 “Sasa kila ukipiga hatua unataka hatua zaidi, kwa hiyo wakati mwingine kelele tunazosikia hizi sio lawama, ni za kutuambiwa sawa tunawashukuru sana , kwa haya mliyofanya lakini tumepata hamu kubwa zaidi ya kupata mengine mengi zaidi.

“Wananchi wanasema maji tumepata uongezeni zaidi wapate maji nyumbani.

Tulikuwa na umeme kila Wilaya, baadae kila kata, sasa wananchi wanataka kila kitongoji, kwa hiyo ni kelele nzuri tu , ni madai mazuri, watu wanataka maendeleo,”amesema Kinana.

Amepongeza hivi sasa kuna barabara za lami zinazounganisha Mkoa na Mkoa,Wilaya na Wilaya na matokeo yake wananchi wanataka barabara katika vitongoji na mitaa yao.”Sio kwamba wanalalamika bali wanakata maendeleo zaidi.

“Baba wa taifa alituambia kupanga ni kuchagua, wa hiyo kazi kubwa tuliyonayo ni kuongeza mapato ya nchi yetu , ili yaweze kukidhi mahitaji.”

SASABU ZA KUMPONGEZA RAIS SAMIA

Katika hatua nyingine, Kinana alieleza sababu za msingi ambazo zinasababisha Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kusifiwa na sababu kubwa ni namna ambavyo ameendelea kutekeleza miradi ya maendeleo na hakuna mradi hata mmoja ambao umesimama.

“Rais Samia Suluhu Hassan anafanya kazi nzuri na wakati mwingine nimeona zimeanza kauli wanasema mbona mnamsifu sana Rais lakini lazima tukubaliane wakato wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hivi kuongoza ni kuonesha njia.

” Ukiwa na kiongozi mzuri , msikivu, mwenye kushirikiana na wenzake wakapanga na mambo yakawa kwanini tusimsifu , lazima tumsifu maana ndio anayetuongoza .Huko nyuma Baba wa Taifa tulikuwa tunasema zidumu fikra za mwenyekiti lakini fikra hazikuwa za Mwenyekiti ni za Chama cha TANU na CCM…

“Kwa sababu gani? Ndio kiongozi wetu anafanya kazi nzuri.Rais Samia kwa muda mfupi sana amefanya kazi kubwa sana, ukimwambia Mkuu wa Mkoa hapa asimame aeleze fedha zilizoletwa katika mkoa huu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita basi nina hakika fedha zinazotolewa kipindi cha Rais Samia inaweza kuwa mara 10, ” amesema

Previous articleBOLT YAZINDUA KITENGO KIPYA CHA UFUATILIAJI WA USALAMA WA SAFARI NCHINI TANZANIA
Next articleNAIBU WAZIRI KHAMIS AWAFARIJI WAATHIRIKA KATESH

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here