Home LOCAL BOLT YAZINDUA KITENGO KIPYA CHA UFUATILIAJI WA USALAMA WA SAFARI NCHINI TANZANIA

BOLT YAZINDUA KITENGO KIPYA CHA UFUATILIAJI WA USALAMA WA SAFARI NCHINI TANZANIA

Dar es Salaam, tarehe 13 Desemba 2023- Kampuni inayoongoza kwa uhitaji wa usafiri barani Afrika Bolt, imezindua vitengo vipya vya ufuatiliaji wa usalama wa safari kwa magari yanayokuwa kwenye mizunguko, na kuwapa madereva na abiria msaada zaidi kutoka kwa timu yao ya usalama ya ndani iliyopewa mafunzo maalum. Bolt sasa itakuwa na uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na abiria na madereva ndani ya programu yao wakati gari litasimama kwa muda mrefu sana ili kuthibitisha kuwa kila kitu kiko sawa. Kitengo hiki kitawapa madereva na abiria chaguo la kupiga simu moja kwa moja huduma za dharura, kushiriki safari, kurekodi sauti au kuomba msaada wa Bolt kwa kubonyeza kitufe kilichopo ndani ya programu.

Bolt inapanga kusambaza vitengo zaidi vya ufuatiliaji wa usalama wa safari ikiwa ni pamoja na kukosewa kwa njia na kuchelewa kukamilika kwa safari. Hii yote ni sehemu ya uwekezaji unaoendelezwa na Bolt katika uboreshaji wa vitengo vya usalama kwenye jukwaa lake, kuwezesha  kutoa msaada zaidi kwa madereva na abiria, na kusaidia kutambua na kuzuia tabia isiyofaa ya madereva na abiria.

Zaidi ya hayo, vitengo vinavyosaidia kuhakikisha usalama wa safari za Bolt kwa madereva na abiria ni pamoja na vitengo vya zana ya usalama ya ndani ya programu kama vile kushiriki safari kwa kuwepo mahali ulipo kwa wakati halisi kwa marafiki na familia, na kitufe cha msaada wa dharura ili kuwasaidia abiria haraka na kwa busara kwa kubonyeza kitufe cha huduma za dharura au washirika wa usalama  kibinafsi ikiwa watawahi kuwa na hofu wakati wa safari.

Takura Malaba, Meneja wa Kanda, Mashariki na Kusini mwa Afrika alisema: “Kwetu sisi Bolt, usalama ndio kipaumbele chetu cha juu na tunawekeza mara kwa mara katika bidhaa na vitengo vipya ili kuendelea kuboresha mfumo wa usalama wa programu ya Bolt, kuwapa madereva na abiria usafiri wa hali ya juu na uzoefu wa kupendeza. Kusambaza vituo vipya vya ufuatiliaji wa usalama wa safari ndio lengo la hivi punde zaidi la juhudi zetu zinazoendelea ili kurahisisha iwezekanavyo kwa madereva na abiria kutafuta msaada ikiwa watawahi kuuhitaji wakati wa safari za Bolt, na kutambua chochote kisicho cha kawaida ili kusaidia. Pia kuzuia kesi za usalama zisizotarajiwa kutokea mara ya kwanza.”

Kuanzisha kwa vitengo vipya vya ufuatiliaji wa usalama wa safari za Bolt ni sehemu ya uboreshaji wa muda mrefu wa ufuatiliaji wa magari yasiyotulia, kuunga mkono juhudi zinazoendelea za timu ya usalama ya Bolt kutambua jambo lolote lisilo la kawaida mara tu safari inapoanza.

Previous articleUREJESHAJI WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KATIKA MJI WA KATESH WAFIKIA ASILIMIA 75
Next articleKINANA: DIRA YA MAENDELEO ITABORESHA PATO LA MTU MMOJA MMOJA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here