Home BUSINESS NCHI WANACHAMA ARIPO ZATAKIWA KUONGEZA NGUVU KWENYE MILIKI UBUNIFU

NCHI WANACHAMA ARIPO ZATAKIWA KUONGEZA NGUVU KWENYE MILIKI UBUNIFU

Waziri wa Sheria na Katiba wa Uganda Bw. Nobert Mao (kulia) wakijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa (katikati) huku Msajili Mkuu kutoka Taasisi ya Usajili Uganda, Bi. Mercy Kainobwisho (kushoto) akifuatilia, wakati wa Mkutano wa 19 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa ARIPO unaofanyika Gaborone Botswana.

Rais wa Botswana Mhe, Dkt Mokgweetsi Eric Masisi amewataka Mawaziri kutoka nchi wanachama wa Shirika la Miliki Ubunifu Kanda ya Afrika (ARIPO) kuhakikisha kuwa wanaongeza nguvu kwenye Miliki Ubunifu badala ya kutegemea Rasilimali pekee.

Rais Masisi ametoa rai hiyo leo tarehe 24 Novemba, 2023 wakati akifungua Mkutano wa 19

wa Baraza la Mawaziri wa Nchi wanachama wa ARIPO unaofanyika Gaborone Botswana.

Amesisitiza kuwa muda umefika kwa nchi za Afrika kuwekeza kwenye maarifa na ubunifu na siyo

kutegemea rasilimali tu na kutolea mfano kuwa katika kipindi cha Uviko 19 nchi za Afrika zilikuja na

bunifu nyingi zikiwa ni pamoja na dawa na vifaa kinga, hivyo bunifu kama hizo zinapaswa kuendelea.

Mhe. Rais pia amewataka Mawaziri kuongeza bajeti zao kwenye masuala ya Miliki

Ubunifu. Katika mkutano huo Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

(BRELA) Bw. Godfrey Nyaisa amemwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji.

Mkutano huo pamoja na mambo mengine umemchagua Mhe. Mmusi Kgafela, Waziri wa Biashara na Viwanda wa Botswana kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa ARIPO kwa kipindi cha miaka miwili.

Mkutano huo wa siku mbili wa Baraza la Mawaziri hufanyika kila baada ya miaka miwili, mkutano uliopita ulifanyika Victoria Fall Zimbabwe mwaka 2021.

Previous articleRAIS SAMIA KATIKA MKUTANO WA KAWAIDA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Next articleBRELA YATAKIWA KUWEZESHA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here