Home BUSINESS BRELA YATAKIWA KUWEZESHA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE

BRELA YATAKIWA KUWEZESHA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI WANAWAKE

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila akimkabidhi cheti Afisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi.Maryglory Mmary, cha kutambua ushiriki wa BRELA katika Maonesho ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi, wilaya ya Kinondoni katika viwanja vya Biafra wakati wa kufunga maonesho hayo leo Novemba 24, 2023 jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam mhe. Albert Chalamila ameitaka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuendelea kuwafikia wajasiriamali wanawake ili kuwezesha biashara zao kutambulika kitaifa na kimataifa.

Mhe. Chalamila ametoa wito huo leo tarehe 24 Novemba, 2023 wakati akifunga Maonesho ya Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi, katika viwanja vya Biafra jijini Dar es Salaam.

Amewataka wajasiriamali wanawake kuchangamkia fursa ya uwepo wa BRELA kwa kurasimisha biashara zao Ili kutambulika kitaifa na Kimataifa.

ameongeza kuwa kwa kurasimisha biashara ni rahisi kuvuka mipaka na kuwa na upekee katika soko ndani na nje ya nchi.

“Uzuri ni kuwa BRELA wapo hapa tumieni fursa hii kupata huduma za sajili mbalimbali ili iwe rahisi kutambulika na taasisi mbalimbali Binafsi na za Umma hii itawawezesha pia kuvuka mpaka wa nchi na kufanya biashara kimataifa”, amesema Mhe. Chalamila.

Pia amewataka BRELA kuendelea kuwafikia wajasiriamali mbalimbali katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuwakumbusha umuhimu wa kurasimisha biashara.

Maonesho hayo ya Jukwaa la Kuwezesha Wanawake Kiuchumi wilaya ya Kinondoni yalianza Novemba 20 na kuhitimishwa leo Novemba 24, 2023.

Previous articleNCHI WANACHAMA ARIPO ZATAKIWA KUONGEZA NGUVU KWENYE MILIKI UBUNIFU
Next articleJAJI MOHAMED CHANDE AMEWATAKA WAHITIMU KUTUMIA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA KUWA FURSA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here