Home BUSINESS MAJALIWA: HALMASHAURI WEKENI MIFUMO YA KURATIBU WANUFAIKA WA TASAF NA VIKUNDI VYA...

MAJALIWA: HALMASHAURI WEKENI MIFUMO YA KURATIBU WANUFAIKA WA TASAF NA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI

Waziri Mkuu waa Jamhuri ya Muungano waà Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akipekua jarida lenye taarifa mbalimbali za TASAF huku akisikiliza maelezo ya Bw. Shedrack Mziray Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakati alipotembelea katika banda hilo kwenye maonesho ya Taasisi za Kifedha yanayofanyika mkoani Arusha katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid  kushoto ni Peter Ilomo Mwenyekiti wa Bodi ya TASAF

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akizungumza na wanufaika mbalimbali wa TASAF ambao ni wajasiriamali wakati alipotembelea katika banda hilo jijini Arusha.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimsikiliza Bi. Tatu Ramadhani mnufaika wa TASAF ambay ni mjasiriamali wakati alipotembelea katika banda hilo jijini Arusha

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa akimshukuru mnufaika wa TASAF Bi. Tatu Ramadhan ambaye ni mjasiriamali mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa mjasiriamali huyo alipotembelea banda hilo.

Bw. Shedrack Mziray Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katikati akifurahia jambo na Fariji Mishael Mkurugenzi wa Tathmini na Mifumo TASAF kulia  na Bi. Zuhura Mdungi Mtaalam wa mawasiliano TASAF.

Meneja wa Kuweka Akiba na Kutunza Uchumi wa Kaya Bi. Sara Mshiu  Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF)  akizungumza na mwandisi wa Fullshangwe hayupo pichani namna TASAF inavyowajengea uwezo na kuwasaidia kaya maskini kwa kutoa mafunzo na kuwaonesha fursa za kiuchumi kwa kushiriki katika maonesho mbalimbali ikiwemo Taasisi za Fedha.

NA: JOHN BUKUKU, ARUSHA

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amezitaka halmashauri zote nchini kuweka mifumo ya kuratibu vikundi vya ujasiriamali ikiwemo Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambao wamekuwa na ufanisi mkubwa katika
ujasiriamali kwa kukuza mtaji mdogo hadi kufikia kiwango cha juu.

Akizungumza leo Novemba 22, 2023 Mkoani Arusha akiwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa tatu wa wiki ya huduma za kifedha, Mhe. Majaliwa, amesema kuwa wakati umefika kwa Kila Wilaya na Mkoa kuwatafutia masoko wajasiriamali pamoja na kubuni maonesho ambayo yataongeza wigo katika biashara.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa TASAF kuna wajasiriamali wazuri ambao wameweza kukuza mtaji mdogo waliopewa na kufanikisha kukuza mtaji na kuanzisha biashara zenye mitaji mikubwa.

“Changamoto iliyopo halmashauri zetu hazijaweza kuwaweka pamoja wajasiriamali wadogo kwa ajili ya kuwaelimisha na kuhamasisha kwa kutafuta maeneo kwa ajili ya kupelekea bidhaa zao” amesema Mhe. Majaliwa.

Wakati huo huo Meneja wa Kuweka Akiba na Kutunza Uchumi wa Kaya Bi. Sara Mshiu amesema Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) umeendelea kuwajengea uwezo na kuwasaidia kaya maskini kwa kutoa mafunzo na kuwaonesha fursa za kiuchumi kwa kushiriki katika maonesho mbalimbali ikiwemo Taasisi za Fedha.

amesema lengo lao ni kunusuru kaya maskini kwa kumsaidia mlengwa katika kuhakikisha wanapiga hatua.

Mshiu  amesema kuwa walengwa ambao wanatoka katika kaya maskini wameshiriki katika maonesho hayo Kwa ajili ya kuonesha bidhaa ambazo wanatengeneza pamoja na kuziuza.

Amesema kuwa wamekuwa wakipewa mafunzo ya uzalishaji wa fedha kupitia bidhaa ambazo wanatengeneza.

“Tuna programu ambayo inawasaidia walengwa kuwa katika makundi ili waweze kujifunza masuala ya kuweka akiba na kuwekeza” amesema

Nae Mnufaika wa TASAF Tatu Ramadhani amesema kuwa yupo katika maonesho hayo kwa ajili ya kuonesha bidhaa ambazo anatengeza baada ya kupata elimu ikiwemo vikapu vya wakinamama, mikanda, bangili kwa kutumia shanga, sabuni pamoja na kava za usukani wa gari.

Amesema kuwa TASAF wamekuwa wakitoa ushirikiano mkubwa katika kufanikisha biashara zao ikiwemo kuwaongezea fedha za mtaji.

Previous articleBRELA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA TAIFA YA NETBOLI YA WANAWAKE- TAIFA QUEENS
Next articleWAZIRI MKUU ATEMBELEA BANDA LA BoT MAONESHO YA TAASISI ZA FEDHA ARUSHA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here