Home SPORTS BRELA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA TAIFA YA NETBOLI YA...

BRELA YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU YA TAIFA YA NETBOLI YA WANAWAKE- TAIFA QUEENS

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bi. Loy Mhando (kushoto), akikabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa timu ya Taifa ya Netboli ya wanawake (Taifa Queens), katika hafla iliyofanyika leo Novemba 22,2023 kwenye Ofisi za BRELA Dar es Salaam. (wa pili kushoto), ni Katibu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Bi. Rose Mkisi, na (wa kwanza kulia), ni Katibu Kamati ya Michezo BRELA Bw. Robert Mashika.

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bi. Loy Mhando (katikati), akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Taifa ya Netboli ya wanawake (Taifa Queens), Leo Novemba 22, 2023 Dar es Salaam. ( Kushoto) ni, Katibu wa Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA) Bi. Rose Mkisi, na ( kulia), ni Katibu Kamati ya Michezo BRELA Bw. Robert Mashika.

Katibu wa Kamati ya Michezo BRELA Bw. Robert Mashika. akizungumza katika hafla hiyo, leo Novemba 22, 2023 Jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM.

Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kwenye sekta ya michezo, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imekabidhi vifaa vya michezo kwa timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens), itakayoshiriki michuano ya Kombe la Afrika yanayotarajia kuanza kutimua vumbi hivi karibuni nchini Botswana.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi vifaa hivyo iliyofanyika leo Novemba 22.2023 katika ofisi za Wakala huyo Jijini Dar es Salaam.  Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bi. Loy Mhando, amesema timu ya Taifa ya Netiboli (Taifa Queens), ni miongoni mwa timu za wanawake zinazofanya vizuri katika mashindano mbalimbali, na kwamba Inahitaji kuungwa mkono na Taasisi, na wadau wote wa michezo nchini.

Amesema kuwa BRELA imekuwa mdau mkubwa katika Sekta ya michezo hapa nchini, na kwamba imekuwa ikiunga mkono jitihada za Serikali  ya Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kushiriki kutoa vifaa mbalimbali vya michezo kama ilivyofanya kwa timu hiyo. 

“Wakala wa Usajili na Leseni (BRELA), imekabidhi vifaa hivi ili kuiunga mkono timu yetu ya Taifa ya Netboli, kwani BRELA ni mdau mkubwa wa michezo na inatambua kuwa michezo ni Afya, Burudani, na pia ni sehemu ya Taasisi kujitangaza.

“Kwa kuzingatia hilo, Taasisi imekuwa ikishiriki katika mashindano mbalimbali ikiwemo inayoandaliwa na Shirikisho la michezo ya Idara za Serikali na Mikoa, (SHIMIWI)” Amesema Bi. Mhando.

Ameongeza kuwa BRELA inatambua kuwa michezo ni Biashara , hivyo kama wadau katika urasimishaji Biashara nchini, wamekuwa wakiunga mkono jitihada za Seikali za kuhakikisha timu za Taifa zinafanya vizuri katika michuano mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Katika hafla hiyo BRELA imekabidhi vifaa mbalimbali kwa timu hiyo ya Taifa Queen, ikiwemo truck suits jozi 25, pamoja na mipira 5 ya Netiboli.

 

Previous articleMAGAZETI YA LEO NOVEMBA 22,2023
Next articleMAJALIWA: HALMASHAURI WEKENI MIFUMO YA KURATIBU WANUFAIKA WA TASAF NA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here