Home LOCAL PROGRAMU YA MAZOEZI KWA WATUMISHI WA WIZARA YAANZA KWA KISHINDO

PROGRAMU YA MAZOEZI KWA WATUMISHI WA WIZARA YAANZA KWA KISHINDO

Na Octavian Kimario, WUSM

Programu maalum ya mazoezi ya kuboresha na kujenga afya ya mwili kwa watumishi wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kwa kishindo Novemba 18, 2023 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Akizungumza mara baada ya kuhitimisha mazoezi hayo Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi. Savera Kazaura amewapongeza watumishi waliojitokeza kwa wingi kushiriki programu hiyo endelevu ya kufanya mazoezi kila Jumamosi kwa lengo la kuimarisha afya za watumishi wa Wizara.

“Nawapongeza kwa kujitokeza kwa wingi kushiriki programu hii maalum ya mazoezi kwa watumishi wa wizara ambayo ni utekelezaji wa maagizo ya viongozi wetu Wakuu wa Wizara, tutahakikisha programu hii inakuwa endelevu ili kujenga afya bora kwa watumishi na kuhamasisha watumishi wengine na jamii kushiriki kufanya mazoezi kuimarisha afya zetu” amesema Bi. Savera.

Naye Mkurugenzi Msadidizi wa Rasilimali Watu Bw. Gideon Malabeja kutoka wizara hiyo amewataka watumishi wahakikishe wanazingatia muda na ratiba ya mazoezi ili kuleta tija kwa washiriki.

Kwa upande wake mshiriki wa mazoezi hayo Bi. Hadija Kisubi ambaye ni Afisa Utamaduni ameeleza kuwa mazoezi yalikuwa mazuri na ameyafurahia akiwasihi na kuwahimiza Wanawake wengine watenge muda wa kufanya mazoezi kila Jumamosi licha ya kuwa na majukumu mengi ili kuungana na watumishi wenzao kuimarisha afya.

Ameongeza kuwa watumishi wanapofanya mazoezi wanamuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye anahimiza watu kufanya mazoezi ili kiumarisha afya na kujenga utimamu wa mwili.

Programu hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Jijinj Dodoma imehusisha mazoezi ya mbio za polepole (jogging), mazoezi ya viungo (aerobic) na mpira wa miguu.

Previous articleWAHITIMU CHUO CHA BoT WAASWA KUWA WAADILIFU NA WAZALENDO
Next articleMHE. RAIS SAMIA AMUAGA RAIS WA ROMANIA MHE.  KLAUS IOHANNIS BAADA YA KUKAMILISHA ZIARA YAKE NCHINI TANZANIA, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here