Home BUSINESS WALIPAKODI WA KATI WAUNDIWA IDARA YAO TRA

WALIPAKODI WA KATI WAUNDIWA IDARA YAO TRA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeunda idara itakayohudumia walipakodi wa kati (MTD), itakayowahudumia wafanyabiashara wenye mzunguko wa mauzo ya Sh. milioni 250 hadi Sh. bilioni 2.5 kwa mwaka.

Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata, akizindua idara hiyo jijini Dar es Salaam jana Novemba 06, 2023, alisema lengo ni kurahisisha huduma kwa wateja.

Alisema kila mfanyabiashara atapewa ofisa mahsusi wa TRA kwa ajili ya kumsikiliza na kufuatilia masuala yake ya kikodi.

Kidata alisema idara hiyo inalenga kuboresha huduma kwa walipakodi hao ili kurahisisha makusanyo ya kodi.

“Sifa za mfanyabiashara kuwa kwenye kitengo cha mlipakodi wa kati ni mauzo ghafi kuanzia Sh. milioni 250 hadi Sh. bilioni 2.5 kwa mwaka…TRA imedhamiria kuboresha huduma kwa walipakodi na kuwaondolea usumbufu,” alisema.

Alisema maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa mamlaka hiyo ni kutofunga biashara au kudai kodi kwa nguvu na kwamba ili kutekeleza agizo hilo TRA imeboresha na kurahisisha mifumo ya ulipaji kodi na ritani ili kuchochea ulipaji kodi kwa hiari.

Kwa mujibu wa TRA, hapa nchini kuna walipakodi wa kati 1,680 ambao watahudumiwa na idara hiyo mpya.
Mwisho.

Previous articleTANZANIA KINARA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BEIJING
Next articleRAIS SAMIA APOKEA UJUMBE TOKA KWA WAZIRI WA ETHIOPIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here