Home LOCAL TANZANIA KINARA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BEIJING

TANZANIA KINARA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA BEIJING

Mgeni Maalum/Rasmi  Dkt. Phumzile Mlambo – Ngcuka (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UN Women na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Jumanne Novemba 7, 2023 katika Viwanja ya TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam.  Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Na Deogratius Temba & Kadama Malunde – Dar es salaam
 
Makamu wa Rais Mstaafu wa Afrika ya Kusini, Dkt. Phumzile Mlambo Ngcuka, amesema Tanzania inaongoza katika kutekeleza maazimio ya Mkutano wa nne wa wanawake duniani uliofanyika Beijing Nchini China mwaka 1995. 
 
Akizungumza leo Jumanne Novemba 7,2023 wakati wa sherehe za ufunguzi wa Tamasha la Jinsia,  na miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Mhe. Dkt. Phumzile ambaye amekuwa pia Mkurugenzi Mkuu wa Shirika linaloshughulikia Masuala ya Wanawake (UNWomen),  ambaye alikuwa mgeni Maalum amesemaMkutano wa Bijing uliofanyika miaka iliyopita 28 uliweka maazimio ambayo Tanzania imeendelea kufanya vizuri kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na nchi zingine. 
 
“Kwa uelewa wangu wa kufanya kazi katika ngazi ya kimataifa, ninaweza kuona mchango wa TGNP katika kujenga uwezo kwa wanawake wa Tanzania kufanya uchambuzi wa masuala ya Kijinsia, ni nchi ya Kolombia na Tanzania pekee ambazo wanawake wamejenga uwezo kwa kiasi kikubwa wa kiuchamnganuzi na kiuchambuzi kuhusu masuala ya Kijinsia” ,amesema Dkt. Phumzile.

 

Dkt. Phumzile Mlambo – Ngcuka akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
 

 

“Mkutano wa Beijing uliipa Tanzania heshima kubwa zaidi, ukizingatia kwamba uliongozwa na Mtanzania ambaye aliweka historia ambayo haitasahaulika duniani kwa kuwa mkutano ule ulizaa maazimio mazito kabisa ambayo yamesababisha mageuzi wa kimifumo, kisera na kisheria katika mataifa mbalimbali lakini pia maazimio yale yamepelekea kuongeza vuguvugu la harakati hizi kuanzia ngazi ya jamii hadi kitaifa, na sasa kuna misamiati mingi ya kukomboa wanawake”,ameongeza Dkt. Phumzile.
 
Amesema dunia itaendelea kuikumbuka Tanzania kwa kile kilichotokea Beijing, chini ya uongozi wa Balozi Getrude Mongela, ambapo hata hivyo nchi inaongoza kwa kuwa na sera zenye mtazamo wa Kijinsia ikiwepo mabadiliko ya kisheria na kimwongozo. 
 
Kwa  upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa UNWomen Tanzania, Hodan Addou akitoa salaam, amesema changamoto za mapengo ya usawa wa Kijinsia bado zipo, ikiwepo Ukatili wa Kijinsia, lakini  kunahitajika nguvu ya mapoja na mshikamano wa mashirika mbalimbali ili kutokomeza kabisa vitendo vya Ukatili wa Kijinsia. 
 
“Tusipofanya jitihada za ziada, itachukua zaidi ya miaka 300 kufikia usawa wa Kijinsia, tunahitaji kujipanga, kushikamana, kuwahusisha wanawake na wanaume kwa umoja wao ili kuzuia mabaya yote ambayo wanawake na watoto wa kike na kiume wanatendewa”, amesema Addou. 
 
Awali akitoa hotuba yake, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Lilian Liundi amesema Tamasha linatoa fursa ya wana jamii hususan wanawake kushirikishana uzoefu, kujadili, kujifunza, kujenga ajenda ya pamoja kuhusu usawa wa jinsia na maendeleo hususani ya namna ya kupanga mikakati ya pamoja ili kusonga mbele kwa pamoja. 
 
“Tunaposhereherekea mafanikio ya harakati zetu kwa miaka 30 ya uwepo wa TGNP, hatuna budi kuipongeza serikali kwa kukubali maoni na mapendekezo kadhaa mbayo tumekuwa tukipelekea na haya ndio yamesababisha Tanzania kuonekana kwamba imetekeleza kwa kiasi kikubwa maazimio ya Beijing”, amesema Lilian.
 
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali amesema lengo kuu la Tamasha la Jinsia ni kupaza sauti za wanawake na kuimarisha ushiriki wao katika lingo za uchumi, jamii, na siasa ambapo wanaharakati wa haki za wanawake kutoka sehemu mbalimbali katika nafasi huru na rafiki wanapata wasaa wa kutafakari maendeleo ya Vuguvugu la Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi (VUWaKi), kusherehekea mafanikio na kujulishana changamoto na mikakati mbadala.

“Katika kuimarisha nguvu za pamoja, Tamasha la Jinsia linatayarishwa na TGNP pamoja na Feminist Activist Coalition (FemAct) na taasisi nyingine za kijamii zenye misimamo inayofanana. Tamasha la Jinsia linatoa fursa kubwa ya kunoa ajenda ya ufeministi na kujenga muafaka juu ya vipaumbele vya ushawishi katika nyanja za haki za wanawake, uwezeshaji, usawa na haki jamii”,amesema.
 
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mgeni Maalum  Dkt. Phumzile Mlambo – Ngcuka (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UN Women na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) leo Jumanne Novemba 7, 2023 katika Viwanja ya TGNP Mabibo Jijini Dar es salaam. Picha zote na Kadama Malunde- Malunde 1 blog
Mgeni Maalum  Dkt. Phumzile Mlambo – Ngcuka (aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la UN Women na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
Mwenyekiti wa Bodi ya TGNP, Gemma Akilimali akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
Mkurugenzi wa TGNP, Lilian Liundi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
Mkurugenzi Mkazi wa UNWomen Tanzania, Hodan Addou akizungumza wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa kwenye Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa kwenye Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
Wanaharakati wa haki za wanawake wakiwa kwenye Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP
 
Picha za kumbukumbu wakati wa ufunguzi wa Tamasha la 15 la Jinsia na Miaka 30 ya TGNP.
 
PICHA ZOTE NA KADAMA MALUNDE – MALUNDE 1 BLOG
Previous articleKATIBU MKUU MADINI APONGEZWA
Next articleWALIPAKODI WA KATI WAUNDIWA IDARA YAO TRA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here