NA: K-VIS BLOG, MLIMANI CITY
MAONESHO ya 7 ya Swahili International Expo Tourism (S!TE) 2023, yaliyoanza Oktoba 6, 2023, kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, yanakamilika leo Oktoba 8, 2023.
Waandaaji wa Maonesho hayo, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) walieleza kuwa lengo la maonesho hayo ni kuwakutanisha wafanyabiashara (wawekezaji) wa hapa nchini, lakini pia wa nje ya nchi.
Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma ni mdau mkubwa kwenye uwekezaji na kupitia Maonesho hayo umeshiriki ili kutangaza fursa zinazotokana na uwekezaji wa Mfuko hususan kwenye majengo makubwa ya Biashara na Makazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodia ya Utalii Tanzani (TTB), Bw. Damas Mfugale, amesema mwaka huu Serikali inategemea kusaini mikataba itakayowezesha ongezeko kubwa la watalii na wafanyabiashara ya utalii kutoka nje wanaotarajiwa kuja nchini.
Mfuko umewekeza kwenye majengo makubwa ya biashara na makazi, kwenye miji yote mikubwa kama vile Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Mtwara na majengo yote hayo yako kwenye maeneo ya kimkakati na yanayofaa kwa shughuli za kiofisi, biashara na hata makazi.