Home BUSINESS RAIS SAMIA KUZUNGUMZA NA DUNIA KUPITIA JUKWAA LA AGRF

RAIS SAMIA KUZUNGUMZA NA DUNIA KUPITIA JUKWAA LA AGRF

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Samia Hassan suluhu Hassan anatarajia kukutana na vijana na kupokea taarifa namna vijana wa Afrika wanavyojihusisha na kilimo na kutumia fursa mbalimbali za kilimo.

Akizumgumza Septemba 6 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema mkutano wa Jukwaa la Mfumo Jukwaa la Chakula Afrika (AGRF ) wadau mbalimbali wamenufaika kwa kujadiliana fursa kwa pamoja.

Amesema wamejadiliana fursa mbalimbali zilizopo ndani na nje ya Bara la Afrika na katikamkutano huo.

“Baada ya mkutano wa vijana maraisi wote watakutana kwenye Summit watakuwa na majadiliano na watapokea taarifa mbalimbali na maadhimio ya mkutano yatasomwa kesho baada ya majadiliano, “amesema Msigwa.

Amesema Rais Dk.Samia anatarajia kuzungumza na vijana namna ambavyo anaona mwelekeo sahihi kwa Bara la Afrika kusaidia vijana kupata ajira kupitia kilimo.

Amsema wanautarajia kuwa na mairais saba wa nchi tofauti watakao hudhuria mkutano wa kesho wa AGRF ambao umehudhuriwa na watu 5000 kutoka nchi 70 za Afrika.

Gerson amesema Rais Dk.Samia anewaalika wageni mbalimbali kwa chakula jioni na ambapo itatolewa tuzo ya chakula Afrika ni kutambua mchango wa kuzalisha chakula.

Amesema moja ya changamoto tulizonazo Afrika ni Upungufu wa chakula baadhi ya maaneo.

Previous articleAGRF YALETA FURSA KWA WADAU SEKTA YA UVUVI NCHINI
Next articleBASHUNGWA AAHIDI KUPAMBANA NA RUSHWA, ATOA MAAGIZO KWA MAMENEJA TANROADS NCHINI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here