Home BUSINESS BEI MAFUTA YA DIZELI YAPANDA ZANZIBAR, ZURA IKITANGAZA VIWANGO MPYA

BEI MAFUTA YA DIZELI YAPANDA ZANZIBAR, ZURA IKITANGAZA VIWANGO MPYA

Na: Halfan Abdulkadir, ZANZIBAR.

Mamlaka ya huduma za maji na Nishati Zanzibar (ZURA) imetangaza bei mpya ya Mafuta huku Dizeli ikipaa kwa asilimia 5.94 kutokea mwezi August hadi Septemba mwaka huu.

Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Septemba 8,2023 kutoka kitengo Cha Uhusiano cha Mamlaka hiyo imesema Bei ya Petroli Kwa Mwezi huu wa septemba Lita 1 itauzwa Shil 2,950 ambapo August ilikuwa ni shil 2,970 ikipungua Shil 20.

“Dizeli Mwezi August ilikuwa lita Moja ni Shil 2,843 ambapo kwa mwezi Septemba ni Shil 3,012 Hii ikiwa ni ongezeko la Shil 169 sawa Asilimia 5.94” ilisema taarifa hiyo.

Aidha Mafuta ya Taa kwa mwezi August na Septemba imeendelea kusalia katika bei Ile Ile ya Shil 2,921 kwa Lita Moja.

Mafuta ya ndege kwa Mwezi wa August ilikuwa ni Shil 2,365 na Septemba imepanda Kwa shil 83 , Hivyo yanauzwa Kwa Shil 2,448 Lita 1.

ZURA imetoa sababu za kupaa kwa Bei ya Dizeli na Mafuta ya ndege ni Kutokana na kuongezeka bei hizo katika Soko la Dunia kwa Asilimia 21, na gharama za Bima na usafirishaji kwa Asilimia 62 tofauti na Mwezi August .

Bei hizo mpya za Mafuta zitaanza kutumika kuanzia Jumamosi ya Septemba 9, 2023.

Itakumbukwa kwamba Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar ( ZURA) imekuwa ikipanga bei za Nishati hiyo kwa kuzingatia mambo mbalimbali yakiwemo Wastani wa mwendeno wa Bei za Mafuta Duniani ( Platts Quotations), Gharama za uingizaji Mafuta katika Bandari ya Dar es salaam na Tanga, Thamani ya Shilingi ya Tanzania kwa Dola za Kimarekani.

Nyingine ni Gharama za usafiri, Bima na ‘Premium’ hadi Zanzibar, Kodi na Tozi za Serikali na Kiwangi cha faida kwa wauzaji wa jumla na rejareja.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here