Home LOCAL RAIS MWINYI: JAMII IZIDI KUONGEZA UPENDO NA KUSAIDIA MAKUNDI MAALUM

RAIS MWINYI: JAMII IZIDI KUONGEZA UPENDO NA KUSAIDIA MAKUNDI MAALUM

Na: Halfan Abdulkadir, Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar Al hajj Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametoa wito kwa jamii kuongeza upendo na ushirikiano hasa kwenye makundi maalum na kuwasaidia kwa kila hali.

Al hajj Dk. Mwinyi, alitoa nasaha hizo leo Septemba 8, 2023 kwenye Msikiti wa Ijumaa Miti Ulaya, Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja , alikojumuika na waumini wa Dini ya Kiislamu kwa ibada ya sala ya Ijumaa.

Al hajj Dk. Mwinyi, amesema jamii inawajibu wa kuyahurumia makundi hayo wakiwemo watoto hususani yatima, wazee, watu Wenye Ulemavu na Wanawake wajane.

Alisema, Waislam wanawajibu wa kuwa karibu na jamii zao kwa kuonyesha upendo hasa kwenye makundi hayo, ambapo aliwaeleza waumini hao kwamba misikiti pia ina wajibu wa kujadili namna ya kuyasaidia kwa wema makundi hayo.

“Ndani ya jamii zetu, tunapaswa kuwahurumia zaidi makundi maalumu, wakiwemo watoto yatima ambao bado hatujaweza kuwalea vizuri”

Aidha, Al hajj Rais Mwinyi aliitaka jamii kuendelea kuhimizana juu ya malezi bora kwa watoto hao, kuwazidishia upendo, kuwajali na kuwatunza vizuri.

Akizungumzia kundi la wanawake wajane, Al hajj Dk. Mwinyi aliwataka viongozi wa misikiti kuona umihimu wa kujadili jinsi ya kuwasaidia kwa wema wajane, watu wenye ulemavu na wazee ili kujenga jamii yenye umoja, upendo na mshikamano.

Naye, Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar, Sheikh Khalid Ali Mfaume aliisisitiza jamii juu ya kuwahurumia wazazi wawili pamoja na wazee wasiojiweza kwa kuongeza upendo kwao na dua njema kwa Mwenyezi Mungu awahurumie kama alivyowahurumia wao walipokuwa wadogo.

Mara baada ya Sala ya Ijumaa, Rais Al hajj Dk. Mwinyi alihudhuria Maziko yaí Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kusini, Marehemu Mgana Zidi Khamis aliyefariki dunia asubuhi na kuzikwa kijini kwao kwa Paje Mkoa wa Kusini Unguja.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 8-2023
Next articleBEI MAFUTA YA DIZELI YAPANDA ZANZIBAR, ZURA IKITANGAZA VIWANGO MPYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here