Home BUSINESS STAMICO YANG’ARA YABEBA TUZO MBILI

STAMICO YANG’ARA YABEBA TUZO MBILI

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limeng’ara katika kikao kazi cha Wenyeviti na Watendaji wa Mashirika ya Umma baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Taasisi za umma zilizofanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji na yenye tija kwa mwaka 2023. (Turn Around Company in Financial and Operational Performance as of June 2023)

Pia STAMICO imenyakua tuzo ya pili katika kundi la mashirika ya umma ambayo yametoa gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. (Outstanding Dividends payment SOE Category as of June 2023.

Tuzo hizo zimekabidhiwa leo jijini Arusha na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyefungua kikao kazi hicho na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dk. Venance Mwasse pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya STAMICO, Meja Jenerali (Mstaafu) Michael Isamuhyo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi tuzo hizo, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu ameipongeza STAMICO na kubainisha kuwa katika miaka miwili iliyopita ilikuwa inafikiriwa kufutwa kutokana na utegemezi lakini sasa wameweza kuchangia hadi gawio kwenye mfuko mkuu wa Serikali.

Previous articleSERIKALI, BUNGE WAAZIMIA KUTOKOMEZA MALARIA IFIKAPO 2030
Next articleMAMA MARIAM MWINYI: WANAWAKE WAJAWAZITO TUMIENI MWANI KUIMARISHA AFYA ZENU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here