Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore akipata maelezo kutoka kwa Unice Kavishe mnufaika wa mafunzo ya ufundi simu kutoka VETA Kipawa Dar es Salaam wakati alipotembelea katika banda la VATA katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo yanayofanyika kwenye viwanja vya Nanenane jijini Mbeya.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore akiangalia ubora wa bidhaa za nguo wakati alipotembelea katika banda hilo kutoka kushoto ni Afisa Habari wa VETA Dora Tesha na katikati ni Meneja Uhusiano VETA , Sitta Peter.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore akipata maelezo kutoka kwa washiriki mbalimbali wa maonesho hayo katika banda la VETA.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Anthony Kasore amesema kuwa wanafunzi wanaohitimu katika vyuo vya ufundi wanatoka na kwenda kufanya kazi kutokana na ujuzi waliopata katika vyuo vya VETA na kuvifanya vyuo hivyo kuwa vya kipekee katika utatuzi wa changamoto za ajira nchini.
Kasore ameyasema hayo katika banda la VETA kwenye maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nane Nane yanayoendelea kwenye viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya.
Amesema kuwa sifa kubwa ya wahitimu wa vyuo vya ufundi wakihitimu kwenda kufanya kazi ni kutokana na masomo yao ni ya vitendo zaidi kuliko kukaririshwa kwa nadharia ndio maana katika maonesho kuna ubunifu wa mashine mbalimbali za kurahisisha shughuli za kilimo.
Amesema kuwa dunia ya sasa inataka wajuzi ndiyo maana tunatoa mafunzo ambayo yanamuwezesha mwanafunzi kufanya kazi, Vyuo vyetu vinaangalia fursa na changamoto zilizopo ili wanapopata mafunzo haya waende kufanyia kazi.
Hii inavipa sifa ya kipekee vyuo vyetu na kuwafanya wanafunzi wetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto za ajira zilizopo kwa vijana nchini.
Kasore amewataka wananchi kutembelea banda la VETA kupata elimu kuhusiana na vyuo vya ufundi pamoja na kutaka vijana na wanawake kuitikia kwenda kusoma.