Home BUSINESS MHE. MASANJA ASIFU UWEKRZAJI WA WADAU SEKTA YA UTALII KATAVI

MHE. MASANJA ASIFU UWEKRZAJI WA WADAU SEKTA YA UTALII KATAVI

·Asisitiza ushirikiano baina ya Serikali na Sekta binafsi katika utoaji huduma za kitalii*

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amezindua hoteli ya Home Ground katika Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi itakayosaidia kukuza Mtandao wa Utalii katika eneo la huduma na malazi kwa watalii wanaokuja nchini.

Akizungumza leo Agosti 6,2023 katika uzinduzi huo, Mhe. Masanja amesema kuwa uwekezaji wa hoteli hiyo unaenda kusaidia Hifadhi ya Taifa Katavi ambayo ni moja kati ya hifadhi ya tano kwa ukubwa nchini ikiwa yenye kilomita za mraba 4,471.

Ameongeza kuwa uzinduzi wa hoteli hiyo ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Serikali na Sekta Binafsi katika utoaji wa huduma za malazi nchini.

“Tukio hili linaonesha dhahiri umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kutoa huduma za kitalii na pia linaunga mkono juhudi thabiti za Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kama alivyoeleza katika uzinduzi wa filamu ya “The Royal Tour ” “tunapenda kuwakaribisha wawekezaji wengine kwani Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kutangaza utalii duniani na kufungua milango kwa nchi nyingi kutembelea Tanzania ” Mhe. Masanja amesema.

Aidha, ametumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa uwekezaji huo mkubwa uliofanyika, huku akisema idadi na viwango vya huduma za malazi imeongezeka.

“Sisi kama Serikali tutazidi kuweka mazingira wezeshi ili kudumisha ushirikiano mkubwa katika kukuza na kuongeza idadi wa watalii wanaofika katika hifadhi hii ya Katavi, wekezeni kwenye huduma za malazi “ amesisitiza Mhe.Masanja.

Naye Mwenyekiti wa Bodi wa Hoteli ya Home Ground, Mhe. William Mbogo amesema ujenzi wa Hoteli hiyo uliogharimu kiasi cha shilingi bilioni 3.5 ulianza mwaka 2019 na unatarajiwa kutumia takribani bilioni 4 mpaka kukamilika kwake.

Amesema uwekezaji huo utasaidia kuchangia katika mapato ya Serikali kwa kodi mbalimbali inayolipa lakini pia umetoa ajira kwa vijana takribani 40 wa Kitanzania.

Mbogo ametumia fursa hiyo kuiomba Serikali kuboresha miundombinu ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi pamoja na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza ndani ya hifadhi hiyo.

Previous articleMKURUGENZI MKUU VETA: UJUZI WANAOUPATA WANAFUNZI WETU NI WA KIPEKEE
Next articleDKT. GURUMO: KUNA MUUNGANIKO KATI YA SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA MAJI NA KILIMO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here