Home BUSINESS DKT. GURUMO: KUNA MUUNGANIKO KATI YA SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA...

DKT. GURUMO: KUNA MUUNGANIKO KATI YA SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA NJIA YA MAJI NA KILIMO

 Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam, (DMI), Dkt. Tumaini Gurumo (kulia), akitoa elimu kwa mwananchi aliyetembelea Banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya Kimataifa ya wakulima Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya. (wa pili kulia), ni Afisa wa Chuo hicho Joyce Mpondaguzi.

(PICHA ZOTE NA : HUGHES DUGILO)

Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), Dkt. Tumaini Gurumo, amesema Muunganiko uliopo kati ya Sekta ya usafirishaji kwa njia ya maji na masuala mazima ya kilimo yamefanya Chuo hicho kufika katika maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane Jijini Mbeya.

Dkt. Gurumo ameyasema hayo Agosti ,7,2023 alipokuwa kwenye Mahojiano na waandishi wa habari katika Maonesho hayo na kusema kuwa, Chuo hicho kipo kwenye Maonesho hayo kutokana kwamba Masuala ya Bahari hayana namna ya kutofautisha na kilimo kwa sababu wakulima wanapovuna mazao yao yanatakiwa yatoke shambani yaingie kwenye maghala yapite kwenye vyombo vya usafirishaji nna kisha yawafikie Wananchi.

“Tumekuwa tukifanya shughuli za kilimo zinafanywa na Watanzania wengi wengi, hivyo huu Muungano tumeona kwamba huwezi kutengenisha kwa sababu wakulima wanapovuna mazao yanatakiwa yatoke shambani yaingie kwenye maghala yapite kwenye vyombo vya usafirishaji ndipo yawafikie Wananchi.

“Hivyo basi  Chuo chetu kinatoa kozi maalumu ambazo zinahusisha usafirishaji kwa njia ya maji, mazao yanawafikia wananchi  waliopo,  katika visiwa yatawafikia kwa njia ya maji hivyo basi tuna kozi inaitwa Shipping and Logistics ambazo zinahusisha kutazama namna gani haya mazao ya kilimo, yanaweza kutoka kule yalipo kupelekwa kwa watumiaji,”amesema Ngurumo.

Ameendelea kusema kuwa mazao hayo yanaposafirishwa kupelekwa nje ya nchi, kutolewa na kupelekwa nje ya nchi,ikiwa kama bidhaa au mazao yanahitaji kusafirishwa kwa wingi na gharama nafuu zaidi, inatumika njia ya maji kuyasafirisha  kwa njia ya maji .

Amesema kuwa wapo kwenye Maonesho hayo kutoa elimu kwa wananchi kukifahamu chuo hicho chenye jukumu kubwa la kutoa ujuzi kwa wananchi katika masuala ya Bahari.

“Tupo katika maonesho haya kwa sababu chuo hiki kinashughulika na mafunzo yanayohusu bahari, lakini masuala ya bahari hayana namna ya kutofautisha na kilimo kwa sababu masuala ya bahari yanazungumiza uchumi wa Bluu umeletwa na unazungumzwa Tanzania na kufanyiwa kazi kwa sababu tunataka kupanua wigo wa ajira, kazi pamoja na maendeleo ya kiuchumi. Ameongeza Dkt. Gurumo.

Previous articleMHE. MASANJA ASIFU UWEKRZAJI WA WADAU SEKTA YA UTALII KATAVI
Next articleMNUFAIKA WA TASAF NA MSOMI WA SHAHADA ATOA USHUHUDA WAKE MAONESHO YA NANENANE MBEYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here