Home BUSINESS MAJALIWA: BoT ENDELEENI KUSIMAMIA TAASISI ZA FEDHA KUSHUSHA RIBA YA MIKOPO

MAJALIWA: BoT ENDELEENI KUSIMAMIA TAASISI ZA FEDHA KUSHUSHA RIBA YA MIKOPO

WAZIRI MKUU wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi (hawamo pichani), katika Banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane, yanayofanyika katika viwanja vya John Mwakangale Agosti 3,2023 Jijini Mbeya 

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Julian Banzi Raphael (katikati aliyekaa), akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Benki Kuu Mbeya, Dkt. James Machemba (kulia), wakisikiliza houba ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (hayumo pichani), alipokuwa akizungumza na wananchi katika Banda la Benki hiyo, kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya. (kushoto), ni Waziri wa Ulinzi wa Tanzania Innocent Bashungwa.

Na: Hughes Dugilo, MBEYA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameiagiza Benki kuu ya Tanzania (BOT) kuendelea kuzisimamia Taasisi za Fedha nchini,  kuboresha riba katika mikopo wanayoitoa.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo Agosti 3,2023 alipokuwa akizungumza na wananchi katika Banda la Benki Kuu ya Tanzania, kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane, yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Amesema kuwa Mabenki yakiwa na riba ndogo itawasaidia  wakulima, wafugaji na wavuvi, kuendeleza shughuli zao, na hivyo kuwataka waangalie uwezekano wa kushusha riba zaidi.

“Nimepitia mabanda ya Mabenki na kuwauliza kuhusu riba. Wengi wao wameshusha kutoka asilimia 12 au 13 ya awali na wamefika asilimia 9. Naamini wataendelea kushusha zaidi,” amesema Waziri Mkuu ambaye alikagua mabanda ya Benki za Azania, CRDB, STANBIC, NBC na TADB.

Na kuongeza kuwa “Wengi walikuwa na riba ya asilimia 20, tukawaambia wakashusha ikafika asilimia 18,wakashusha ikawa asilimia 17,na badae ikawa asilimia 15, wakaja kukwama kwenye asilimia 12, hivyo basi nimefurahi sana kukuta wameshuka wapo kwenye 9,na Matumaini yangu watashuka zaidi, ameongeza Mhe .Majaliwa.

Amesema uwepo wa Mabenki katika Maonesho hayo kunawapa fursa wananchi hususani wakulima, kufahamu namna watakavyonufaika na mikopo ilitolewayo na Taasisi za Fedha, ili kuanzisha na kuendeleza shughuli zako za kilimo, ufugaji na uvuvi.

BoT inashiriki Maonesho ya Nanenane mwaka huu, ikitoa elimu ya Fedha na shughuli wanazofanya kwa wananchi mbalimbali wanaotembelea katika Banda lao.

(PICHA MBALIMBALI ZA WATUMISHI WA BoT WAKITOA HUDUMA)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here