Home BUSINESS CHUO CHA BoT: TUMEJIANDAA KIKAMILIFU KUWAPOKEA WANAFUNZI

CHUO CHA BoT: TUMEJIANDAA KIKAMILIFU KUWAPOKEA WANAFUNZI

Mratibu wa Mafunzo Chuo Cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT)) Tulla Mwigune, (kushoto), akizungumza na wanafunzi waliotembelea Banda la Benki hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale  Jijini Mbeya.

Mratibu wa Mafunzo Chuo Cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT)) Tulla Mwigune, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati wa mahojiano yaliyofanyika katika Banda la BoT, kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Mwandishi wetu, MBEYA

Mratibu wa Mafunzo Chuo Cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT)) Tulla Mwigune, amesema kuwa Chuo hicho kimejiandaa kikamilifu katika kuhakikisha wanafunzi wote watakaopata nafasi ya kujiunga na Chuo hicho mwaka wa masomo 2023/2024 wanapokelewa  bila changamoto yeyote.

Mwigune ameyasema hayo leo Agosti 4, 2023 wakati  akizungumza na  waandishi wa habari kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Nanenane yanayofanyika kwenye viwanja vya John Mwakangale  Jijini Mbeya.

Amesema kuwa, baada ya kupokea maombi hayo watayachakata ili kuwapata wale wenye sifa ya kujiunga na Chuo na kupatiwa taarifa rasmi kwa ajili ya kuanza maandalizi.

“Baada ya kupokea maombi tutayachakata, wale ambao wamechaguliwa watatumiwa taarifa maalum kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kujiunga na Chuo” amesema Mwingine.

Ameeleza, wapo kwenye maonesho hayo ili kutoa elimu kwa wananchi na kwamba, kuna vijana wengi wamekuwa wakifika kupata maelezo juu ya kozi mbalimbali wanazozitoa, na kufahamu fursa nyingine zinazopatikana katika Chuo hicho.

“Wanafunzi wengi wamekuwa na changamoto ya kutojua kozi za kusoma, mfano kuna mwanafunzi anaweza kusema ili awe mhasibu lazima asome kozi za uhasibu, lakini haiko hivyo, ili uweze kuwa Afisa wa Benki kuna kozi ya Benki yenyewe ambayo ndani yake unasoma vitu halisia  vinafanyofanyika Benki

“Tunavyoongelea Benki kuna vitengo mbalimbali, tukianza na huduma kwa mteja, kuna sehemu inayohusika na mikopo, pia kuna uhasibu ambao vijana wengi ndi wanaijua sasa lakini haya maeneo yote mtu anaweza akasoma kupitia hii kozi ya Benki, hivyo basi tunawakaribisha wanafunzi katika chuo chetu ili kupata elimu hiyo” ameeleza Tulla.

Aidha amesema kuwa Benki kuu imefanya uwekezaji mkubwa wa miundombinu mbalimbali chuoni hapo, ambapo  wanafunzi wote watakaopata nafasi ya kusoma katika Chuo hicho wataweza kusoma kwa utulivu na kwamba, Chuo kimejitosheleza kwa madarasa ya kutosha pamoja na Maktaba ya kisasa yenye vitabu vipya, na maeneo tulivu ya kujisomea.

Previous articleMAJALIWA: BoT ENDELEENI KUSIMAMIA TAASISI ZA FEDHA KUSHUSHA RIBA YA MIKOPO
Next articleBoT YATOA RAI KWA WANANCHI KUTUNZA FEDHA KUEPUKA UCHAKAVU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here