Home BUSINESS VETA MOSHI YATAMBULISHA ‘ECCENTRIC PRESS MASHINE’ KUSAIDIA VIJANA

VETA MOSHI YATAMBULISHA ‘ECCENTRIC PRESS MASHINE’ KUSAIDIA VIJANA

DAR ES SALAAM 

Katika kuhakikisha kuwa Vijana wanaomaliza mafunzo ya Sfundi Stadi wanajikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira, Chuo cha VETA Moshi kimetengeneza Mashine inayounda zana ambazo zinatumika kuzalishia bidhaa kwaajili ajili ya viwandani.

Akielezea kuhusu Mashine hiyo, mwalimu Irene Muro kutoka chuo cha VETA Moshi, amesema Chuo chao kimebuni Mashine hiyo ili kuwaandaa wanafunzi wao kujiajiri pindi watakapohitimu mafunzo yao.

“Sisi tunamfundisha mwanafunzi kutengeneza zana ila tumeona maswali ni mengi kwamba unamfundisha mwanafunzi kuandaa zana za uzalishaji lakini anaenda kuzalisha kwa kutumia mashine zipi wakati mashine hazipatikani mtaani kwa urahisi?, Hivyo basi tukakaa na wanafunzi , tukawaekeza jinsi ya kutengenezea mashine ili kusudi akimaliza kusoma akiweza kutengeneza aweze pia kuwa na mashine yake mwenyewe.

“Mashine ijulikanayo kama ‘Eccentric Press Machine’ ambayo tumeitengeneza wenyewe walimu pamoja na wanafunzi kwa ajili ya kuzalishia zana mbalimbali za viwandani kama vile, Komeo, Bawaba, Sufuria, Sahani za Bati na bidhaa nyinginezo ” ameeleza Mwalimu Muro.

Ametoa wito kwa vijana wa kitanzania kujiunga na vyuo vya VETA vilivyoenea kote nchini na kwamba, kwa kufanya hivyo watakuwa wamepiga hatua kubwa ya kujiajiri wenyewe na kumudu gharama za maisha.

Previous articleWIZARA YA MALIASILI YAJA KIDIGITALI SABA SABA
Next articlePURA YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here