Na: Mwandishi wetu, Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza Watumiaji Huduma za Usafiri wa Anga nchini, TCCIA, CCCC Innocent Kyara amewasihi wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutekeleza miradi mbalimbali kwaajili ya maendeleo ya nchi.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Julai 7,2023, kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kamataifa (sabasaba) yanayoendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Juliaus Nyerere Jijini Dar es Salaam, alipokuwa kwenye banda lao kwaajili yakutoa elimu kwa wananchi mbalimbali waliotembelea katika banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho hayo.
Amesema kwa mujibu wa Kaulimbiu ya mwaka huu, isemayo Tanzania ni mahali sahihi na salama kwa Biashara na Uwekezaji, imeenda sambamba na dhamira yao ya dhati ya kuisaidia Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wananchi kutumia fursa zinazopaatikana katika miradi inayotekelzwa na wawekezaji hapa nchini.
“Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kutafuta wawekezaji kwa usiku na mchana kwa kuwa wanafungua nchi yetu, Raisi wetu Samia Suluhu Hassan anapambana kutafuta fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali, sasa ni wajibu wetu kumuunga mkono kwa kuchangamkia fursa na kufanya kazi kwa bidii.
“Si vyema kubeza na kupinga kwenye mitandao ya kijamii, sana sana kwa Sasa sisi ni wajibu wetu kufungua akili,macho, mawazo na masikio yetu kuangalia ni namna gani kila Mtanzania Mmoja Mmoja anaweza akanufaika Moja kwa Moja na hivi karibuni shirika la Ndege kupitia Serikali walileta ndege ya mizigo,Sasa ukiwa kama mwananchi unapaswa kuumiza kichwa ni namna gani utachangia katika uendeshaji wa hili shirika,” amesema Kyara.