Home BUSINESS DIB: ZAIDI YA ASILIMIA 98 YA WATEJA SEKTA YA FEDHA WANA KINGA...

DIB: ZAIDI YA ASILIMIA 98 YA WATEJA SEKTA YA FEDHA WANA KINGA YA BIMA

Afisa mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana Bi. Joyce Shala, akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) wakati wa mahojiano maalum juu ya majukumu yanayotolewa na Bodi hiyo, chini ya usimamizi wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Juliaus Nyerere Jijini Dar es salaam.

Afisa Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana Bi. Joyce Shala (kushoto), akifafanua jambo wakati wa Mahojiano hayo, katika Banda la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam. (kulia), ni Mhasibu wa Bodi ya Bima ya Amana Beatrice Kalanga.

Mhasibu kutoka Bodi ya Bima ya Amana Beatrice Kalanga, akifafanua jambo na kuwakaribisha wananchi kutembelea Banda la BOT ili kupata elimu juu ya Bima hiyo, katika Maonesho ya Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Afisa Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana Bi. Joyce Shala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wenzake wa BoT. (kushoto), ni Mhasibu kutoka Bodi ya Bima ya Amana Beatrice Kalanga, na (kulia), ni Afisa habari wa BoT, Graciana mahega.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Bodi ya Bima ya Amana imesema kuwa zaidi ya asilimia 98 ya wateja waliopo katika benki na tasisi za fedha nchini wana kinga ya bima ya amana.

Pia, wateja wote wenye viwango vya fedha kuanzia shilingi moja (1) mpaka shilingi milioni 7.5 wanaweza kupata pesa yao pale benki au taasisi ya fedha inapofilisika.

Hayo yamebainishwa na Afisa Mwandamizi Bodi ya Bima ya Amana, Bi. Joyce Shala, alipozungumza na waandishi wa habari kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam namna Bodi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.

Amesema kuwa kama zilivyo Bodi za Bima za Amana nyingine ulimwenguni, serikali iliunda Bodi ya Bima ya Amana nchini, kwa lengo la kuwalinda wenye wateja wenye amana kutokana na athari ya kupoteza amana zao endapo kunapotokea changamoto inayopelekea Benki au Taasisi ya fedha kuanguka.

“Bodi yetu ya Bima ya amana ina jukumu la kusimamia mfuko wa Bima ya Amana (Deposit Insurance Fund – DIF), ili kuwepo na Bima ya Amana inayotoa kinga kwa wenye Amana katika Benki au Taasisi ya fedha inapofilisika, au kuwekwa katika ufilisi.

“Kwa sasa Bodi yetu inatoa kiwango kipya cha fidia ambapo kuanzia mwezi Februari 2023, ikitokea Benki au Taasisi ya fedha imeanguka au kufungwa, watapata kuanzia Shilingi moja (1) mpaka milioni saba na laki Tano, (7,500,000)”

Alisema kuwa Tanzania ni mahali salama kufanya biashara na uwekezaji kwani fedha zao ziko salama chini ya usimamizi wa Benki Kuu yenye jukumu la kusimamia sekta zote za fedha.

Tunawahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji kuwa Tanzania ni mahali sahihi pa kufanyia Biashara na Uwekezaji kwani fedha za watanzania ziko salama chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), yenye jukumu la kusimamia sekta zote za fedha nchini, ikiwemo Bodi ya Bima ya Amana (DIB) kwaajili ya kukinga Amana za wenye Aamana zao pale ambapo kwa bahati mbaya Benki imefungwa” ameeleza Bi. shala.

Ameongeza kusema kuwa Bodi hiyo pia ina jukumu la kusimamia ufilisi wa Mabenki au Taasisi ya fedha pale ambapo Bodi ya Bima ya Amana imeteuliwa na Benki Kuu ya Tanzania kufanya kazi hiyo.

Kwa sasa Bodi ya Bima ya Amana inaendelea na ufilisi wa zilizokuwa Greenland Bank (T) Limited, Delphi’s Bank (T) Limited, FBME Bank Limited, Mbinga Community Bank Plc, EFATHA Bank Limited, Njombe Community Bank limited, Kagera Famers’ Cooperative Bank limited, na Meru Community Bank Limited

Previous articleKAMISHNA JENERALI MADAWA YA KULEVYA NA MWANAMFALME WA ZULU AFRIKA KUSINI WATEMBELEA BANDA LA TMDA
Next articleTCAA CCC YATOA ELIMU KWA WANANCHI MAONESHO YA SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here