Home BUSINESS TAA YABORESHA NA KUJENGA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI

TAA YABORESHA NA KUJENGA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI

Na: Neema Adriano, DAR ES SALAAM

Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege TAA imeendelea kujenga Viwanja vipya na kuboresha Viwanja vya ndege ili kupokea wawekezaji wanaokuja kuwekeza Nchini.

Akizungumza kwenye Viwanja vya Mwalimu Juliaus Kambalage Nyerere kwenye maonyesho ya 47 ya biashara, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege TAA, Mussa Mbura Amesema kuwa mamla hiyo imekasimiwa na mamlaka ya kuendesha Viwanja vya ndege vya Serikali na kuendeleza kuendesha na kusimamia kwa niaba ya Serikali ambayo unaendesha Viwanja 58 ambavyo vyote vipo Tanzania bara

“Vipo Viwanja vikubwa ambavyo vimekuwa vukitumiwa sana na Serikali kusafirisha abiria kutoka ndani na nje ya Nchi, ikiwemo Kiwanja Cha Mwalimu Juliaus Kambalage Nyerere na kama mjuavyo kauli mbiu inayosema Tanzania ni mahali sahihi biashara na Uwekezaji,kwa sababu wawekezaji Hawa ili waweze kuja Nchini lazima watumie Viwanja vya ndege na ni asilimia 60 ya wageni hufika Nchi kwa kutumia Viwanja hivyo.

“Baada ya ugonjwa wa uviko 19,tunapokea wageni,wawekezaji wanaoingia Nchini na kwa kulitambua hilo Serikali yetu ya Raisi Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Viwanja vipya na kwa sasa tuna mradi mkubwa kule msalato.

“Kufuatia filamu yetu ya. Royal Tour imefanya wageni wengi waweze kuja kwa ajili ya kuangalia vivutio mbalimbali vilivyopo Nchini kwa hiyo Viwanja vyetu viko salama pamoja na kuwa na taa ili kurahisisha wasafikiri kusafiri na kufika muda wowote,” amesema Mbura.

Hivyo basi niwaombe Watanzania wote kwa ujumla wafike katika Banda letu ili waweze kupata elimu na kutangaza fursa ambazo zipo katika Viwanja vya ndege

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here