Home LOCAL MSAMA AWAASA WABUNGE, VIONGOZI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

MSAMA AWAASA WABUNGE, VIONGOZI KUMUUNGA MKONO RAIS SAMIA

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo, Julai 6, 2023, Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Neema Adriano, DAR ES SALAAM.

Viongozi mbalimbali wakiwemo wabunge, wameshauriwa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake anazofanya katika kuhakikisha uchumi wa nchi unakuwa.

Akizungumza mapema leo,Julai 6, 2023, Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama, amesema kuwa Wabunge pamoja na viongozi wengine wanapaswa kuwa imara katika kupeperusha sera nzuri za Tanzania, na kwamba, hawapaswi kubaki nyuma katika kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais.

“Watu wote ambao wenye nia mbaya na nchi yetu, lazima tupambane nao bila kuwaogopa wala kuwaonea haya. Nchi yetu ni ya kila mtamzania, na ana haki ya kupambana kuhakikisha Amani, Utulivu na mshikamano tulionao unaendelea kuwepo.

“Rais anafanya kazi kubwa sana, mambo mengi yalikuwa hayaendi, lakini sasa mambo yanaenda vizuri sana, wawekezaji wakubwa, wadogo na wa kati wanakuja kuwekeza nchini kwetu, haya yote ni matunda yatokanayo na yeye kutembelea kwenye Nchi mbalimbali za kigeni kuunganisha Biashara ili kukuza uchumi wa nchi” amesema.

Previous articleTAA YABORESHA NA KUJENGA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI
Next articleMSD YASHAURIWA KUENDELEZA MIKAKATI UPATIKANAJI WA BIDHAA ZA AFYA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here