Home BUSINESS BRELA YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA 47 YA BIASHARA YA KIMATAIFA, DAR ES...

BRELA YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA 47 YA BIASHARA YA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar uuhu Dkt. Hussein Ali Mwinyi akikabidhi tunzo ya mshindi wa kwanza  katika ubunifu katika biashara Mwakilishi wa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Andrew Mkapa  wakati wa ufungaji kilele cha Maonesho ya 47 ya Biashara Kimataifa Dar es Salaam (DITF) katika Viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi akisalimiana na kukaribishwa Katika Banda la BRELA, na Kaimu Mtendaji Mkuu wa BRELA  Bw. Andrew Mkapa akimuwakilisha Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Bw. Godrey Nyaisa, mara baada ya kuwasili katika Banda la Taasisi hiyo kujionea shuguli mbalimbali zinazofanywa na Wakala huyo kwenye maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa JULAI 13,2023 Jijini Dar es Salaam.
   Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi,  akipata maelezo ya namna Mfumo wa usajili kwa Njia ya Mtandao (ORS) (haupo pichani) unavyofanya kazi. Maelezo hayo aliyapata kutoka kwa Bw. Andrew Mkapa, aliyemwakilisha Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili na Biashara Leseni (BRELA) alipotembelea  banda la BRELA kwenye Maonesho ya 47 Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam leo tarehe 13 Julai, 2023 alipofunga maonesho hayo.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Mwinyi, akimkabidhi Mfanyabiashara cheti cha Usajili wa Jina la Biashara alipotembelea  Banda la BRELA kwenye Maonesho ya 47 Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imeibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha Uwezeshaji wa Ukuzaji wa Biashara na Uwekezaji na kuibuka mshindi wa nne katika kipengele cha Banda Bora katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam yaliyofanyika katika uwanja wa Mwalimu J.K Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.

Tuzo za ushindi huo zimetolewa tarehe 13 Julai 2023 na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, wakati wa kufunga maonesho hayo.

Katika kipengele cha Uwezeshaji wa Ukuzaji wa Biashara na Uwekezaji waliochukua nafasi ya pili ni Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wakifuatiwa na Mamlaka ya Rufaa ya Manunuzi ya Umma (PPAA),wakati kwa upande wa Mabanda bora waliochua nafasi ya kwanza ni banda la Algeria, ikifuatiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) nafasi ya tatu ilichukuliwa na Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT).

Ushindi wa nafasi ya kwanza kwa BRELA ni mwendelezo wa jitihada za Taasisi katika kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja na wadau wake, ambapo katika Maonesho ya 46 BRELA ilipata ushindi wa nafasi ya pili katika kipengele hicho hicho cha Uwezeshaji wa ukuzaji wa Biashara na Uwekezaji.

Kabla ya kufunga Maonesho hayo, Rais Mwinyi alitembelea Banda la BRELA ambapo alipata fursa ya kuona jinsi Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) unavyofanya kazi. Pia alitumia nafasi hiyo kukabidhi Cheti cha Usajili kwa mmoja wa wafanyabiashara waliofika katika Banda la BRELA na kupata huduma ya usajili wa papo kwa papo zilizotolewa wakati wa Maonesho hayo kiwanjani hapo.

Previous articleDk. KIKWETE KUWAAGA WAPANDA MLIMA 61 KAMPENI YA GGML KILICHALLENGE -2023
Next articlePURA YAPONGEZWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here