Home BUSINESS PURA YAPONGEZWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI

PURA YAPONGEZWA KUFANYA KAZI KWA UFANISI

Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi (PURA), Joan Karama (kulia) akimsikiliza Mjiofizikia wa Taasisi hiyo Josephine Jumanne (kushoto), alipokuwa akitoa maelezo kuhusiana na kifaa maalum cha Uhalisia tepe, (Virtual reality – VR) wakati wa Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ,(Sabasaba) yaliyomalizika rasmi Julai 13,203 Katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi wetu, DAR ES SALAAM

Wananchi mbalimbali waliotembela Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yaliyomalizika Julai 13, 2023 wamepongeza ufanisi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu (PURA),  kwa namna inavyotekeleza majukumu yake mbalimabali ikiwemo utafiti wanaofanya katika upatikanaji wa Nishati ya Gesi na Mafuta.

Wakiongea kwa nyakati tofauti walipokuwa katika Banda la Taasisi hiyo, baadhi ya wananchi hao waliipongeza PURA kwa kazi kubwa wanayofanya hasa katika utafiti wa Gesi na Mafuta.

PURA imeshiriki Maonesho ya Sabasaba mwaka huu kutoa elimu kwa wananchi namna wanavyotekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.

Moja ya tukio lililowavutia wengi, ni uwepo wa kifaa maalum Virtual reality (VR), kinachotumika kuonesha ramani yenye eneo la mradi patakapfungwa mitambo ya kuchakata rasilimali ya gesi.

Kifaa hicho kinaonesha muonekano wa mradi wa LNG pale utakapokamilika. Kinaonesha ramani yenye eneo la mradi (nchi kavu patakapofungwa mitambo ya kuchakata, na baharini kwenye rasilimali ya gesi); uzalishaji wa gesi kwa visima kutoka kwenye miamba chini ya sakafu ya bahari; usafirishaji wa gesi hiyo kutoka visima mbalimbali, ukusanywaji wa gesi kutoka kwenye visima kuingia kwenye bomba litakaloisafisirisha hadi nchi kavu mahali penye mitambo, mitambo ya kuchakata gesi kuwa LNG, na upakiaji wa LNG kwenye meli maalumu kuisafirisha kwenye masoko nje ya nchi.

(PICHA MBALIMBALI ZA  BAAHI YA WATUMISHI WA PURA)

Previous articleBRELA YAIBUKA KIDEDEA MAONESHO YA 47 YA BIASHARA YA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM
Next articleDP WORLD HAITAMILIKISHWA ARDHI YA TANZANIA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here