Home BUSINESS TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) YAPIGA KAMBI SABASABA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) YAPIGA KAMBI SABASABA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

Afisa Uhusiano Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dorothy Natale (kushoto) akitoa Elimu kwa wananchi waliotembelea katika Banda la Taasisi hiyo, kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Juius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

TET inashiriki maonesho ya Sabasaba mwaka huu, kwa lengo la kutoa Elimu kwa wananchi na watu mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo, wakiwa na Vitabu vya Kiada kuanzia elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, Vitabu vya hadithi za watoto, Miongozo ya kufundishia, Muhtasari na machapisho mbalimbali.

TET Wanapatikana katika Jengo la Jakaya Kikwete chumba namba 1, 2 na 3.

Afisa Uhusiano Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dorothy Natale (kushoto) akimkabidhi kipeperushi mwananchi aliyetembelea Banda la Taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Afisa Uhusiano wa TET, Dorothy Natale (kushoto) akishuhudia wageni waliotembelea kwenye maonesho hayo, wakitia saini katika kitabu maalum cha wageni waliofika kwenye Banda lao.

Afisa Mauzo TET Anold Musaroche (kulia), akikagua vitabu tayari kwaajili ya kumkabidhi mteja aliyefika kwenye Banda lao kufanya manunuzi.

Afisa Mauzo TET Anold Musaroche (kulia), akimkabidhi mteja vitabu baada ya kufanya manunuzi.

Afisa Uhusiano Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dorothy Natale (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wenzake katika Banda lao. (wa kwanza kushoto), ni Afisa Mauzo TET Anold Musaroche, (wa pili kushoto), ni Mkuza Mitaala wa Taasisi hiyo, Charles Manyama, na (kulia), ni Mhariri wa vipindi vya Televisheni TET, Marko Sallu.

(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Previous articleWAFANYABIASHARA KUTOKA AFRIKA KUSINI WATEMBELEA SIDO MAONESHO YA SABASABA
Next articleMATUKIO KATIKA PICHA: MAHAKAMA YATOA ELIMU KWA WANANCHI SABASABA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here