Home LOCAL MATUKIO KATIKA PICHA: MAHAKAMA YATOA ELIMU KWA WANANCHI SABASABA

MATUKIO KATIKA PICHA: MAHAKAMA YATOA ELIMU KWA WANANCHI SABASABA

Hakimu Mkazi wa Mahakama Inayotembea,Mhe. Simon Laizer akitoa maelezo  kuhusu fomu ya mgawanyo wa mali za  marehemu kwa wananchi waliofika kupata huduma hiyo(hawapo pichani)

Afisa Kumbukumbu  wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Mariam Jacob (aliyesimama) akitoa maelezo ya jinsi kujaza fomu ya orodha ya mali za marehermu kwa Bi. Mwajabu Difika(aliyevaa ushungi wa maruni) na Bi. Mwasha Rashid  ndani  ya Mahakama Inayotembea iliyopo  banda la Mahakama  ya Tanzania kwenye  Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius  K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Hakimu Mkazi wa Mahakama Inayotembea, Mhe. Simon Laizer(katikati) akikagua fomu hiyo.

Mawakili kutoka Chama cha  Wanasheria Tanganyika(TLS) Chapter ya Ubungo wakitoa huduma ya kiapo cha kutokuwa na ajira kwa Bi. Zawadi  Selemani(kulia) na (kulia aliyevaa nguo nyeusi) ni Bi. Oliver Katamwa kwenye banda la Mahakama ya Tanzania katika maonesho hayo.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Watoto Kisutu, Mhe. Orupa Mtae akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw. Martin  Kamisha(aliyenyoosha mkono) ambaye anataka kufahamu taratibu za kuasili mtoto kwenye banda la Mahakama ya Tanzania katika maonesho hayo.

(Picha na  Magreth Kinabo- Mahakama)

 

 

Previous articleTAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET) YAPIGA KAMBI SABASABA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI
Next articleOFISI YA WAZIRI MKUU YAWAPIGA MSASA WASTAAFU WATARAJIWA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here