Home BUSINESS PROFESA MKENDA KUFUNGUA MAONESHO YA NANE YA TAFITI NA UBUNIFU UDSM

PROFESA MKENDA KUFUNGUA MAONESHO YA NANE YA TAFITI NA UBUNIFU UDSM

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda anatarajia kufungua maonesho ya nane ya Utafiti na Ubunifu yanayotarajia kuanza Mei 23 – 25, 2023 katika Viwanja vya Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Utafiti, Prof. Nelson Boniface amesema maonesho hayo yenye kauli mbiu “Utafiti na Ubunifu kwa Ustawi wa Uchumi – jamii nchini Tanzania”

Prof. Nelson Boniface amesema kuwa maonesho hayo yatataguliwa na ufunguzi ambapo wazungumzaji watakuwa ni Letice Rutashobwa ambaye ni mbobezi katika masuala ya biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Michael Shirima mwenyekiti na Mwanzilishi wa Presicion Air Tanzania

Amesema kuwa katika maonesho hayo ya nane wanatarajia kuonesha miradi 99 iliyotokana na maonesho yalifanyika katika ngazi ya vitengo ambapo jumla ya miradi 350 na wakachagua hiyo 99.

“Malengo ya Tafiti hizi ni kuwavutia wanataaluma kutoka chuo chetu na taasisi nyingine zinazohusiana na Taaluma Pamoja na utafiti na watu wote wa serikalini ikijumlisha wenye viwanda kuja kushuhudia tafiti na bunifu zao wanazofanya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,” amesema Prof. Nelson Boniface.

Ameongeza kuwa tafiti zote zinazofanywa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zinalengo la kuboresha maisha ya Watanzania hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa wingi kuhudhuria maonesho hayo ili waweze kujifunza mambo mbali mbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here