Home BUSINESS BoT YAHAMISHA MALI NA MADENI YA YETU MICROFINANCE PLC KWENDA NMB

BoT YAHAMISHA MALI NA MADENI YA YETU MICROFINANCE PLC KWENDA NMB


Kwa mamlaka iliyopewa chini ya kifungu cha sheria cha 56 (1) (g)(i) na (iii) cha  Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, mnamo tarehe 12 Disemba  2022 Benki Kuu ya Tanzania iliiweka chini ya usimamizi wake Yetu Microfinance Bank  Plc kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili ya mtaji na ukwasi.  Shughuli za kawaida za biashara za Yetu Microfinance Bank zilisimamishwa  kuiwezesha Benki Kuu kutathmini hatua stahiki za kuchukua.  

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuujulisha umma kuwa, kwa mujibu wa kifungu  cha 59(4) cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 mchakato wa  kupata suluhisho la Yetu Microfinance Bank Plc umekamilika, na uhamishaji wa mali  na madeni kwenda benki nyingine ndio hatua stahiki iliyofikiwa. Hivyo, kwa mujibu  wa kifungu cha 58(2)(h) cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006,  Benki Kuu ya Tanzania imehamisha mali na madeni ya Yetu Microfinance Bank Plc  kwenda NMB Bank Plc kuanzia tarehe 24 Mei 2023. 

Wenye amana na wadai wengine wa Yetu Microfinance Bank Plc watapewa  taarifa ya namna na siku watakayoanza kupata huduma za kibenki kupitia benki  ya NMB. Wakati huo huo, wateja wote wenye mikopo wanatakiwa kuendelea  kulipa marejesho yao kwa mujibu ya mikataba yao ya mikopo.  

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda  maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika  sekta ya kibenki. 

GAVANA 

BENKI KUU YA TANZANIA 

Previous articleBENKI YA NBC YAZINDUA RASMI  USAJILI WA MBIO ZA  NBC DODOMA MARATHON 2023
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI LEO MEI 24,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here