Home LOCAL WANANCHI WAPATE ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE –...

WANANCHI WAPATE ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE – PROF. MAKUBI

Na. WAF – Dodoma

Serikali imeagiza kutolewa kwa elimu ya bima ya afya kwa wote kuelekea kipindi hiki cha kusomwa tena Bungeni kwa Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote.

Hayo yameelezwa leo na Katibu Mkuu, Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi katika kikao maalumu kati ya Wizara ya Afya na Watendaji Wakuu wa Taasisi zilizopo chini yake ili washiriki kikamilifu katika utoaji elimu kwa wananachi kwa lengo la kuongeza uelewa wa dhana na umuhimu wa kila mwananchi kuwa na bima ya afya. Katibu Mkuu ameelekeza suala la utoaji Elimu hii ni mtambuka na lazima kushirikisha Wizara na Taasisi zingine za Serikali na binafsi.

“Tumeandaa Mpango Harakishi na Shirikishi ambao utawahusisha viongozi wote wa Wizara nyingi za serikali na Taasisi zake na dhamira mahususi ya mpango huo ni kuongeza uelewa na hamasa kwa wananchi kuhusu uelewa wa mambo muhimu yatakayotekelezwa baada ya Sheria inayopendekezwa kutungwa”, amesema Prof. Makubi.

“Amewahimiza Watendaji hao kwenda kushirikiana na Ofisi za Wakuu wa Mikoa/Wilaya na timu zao pamoja na taasisi zilizopo katika mkoa/wilaya husika ili kutoa elimu ya dhana ya bima ya afya kwa wote.

“Ni muhimu kuyafikia makundi ya wananchi wa kawaida ikiwa ni pamoja na wafanyabiashara, vyama vya ushirika, wakulima, wafugaji, viongozi wa dini, serikali za mitaa, mama ntilie, wamachinga na bodaboda tunawafikia kwa kuwapa elimu lengo kubwa ni kuwaomba wakapande mbegu na kutoa elimu zaidi ili kulifikia kundi kubwa la wananchi wenye kuwa na elimu kuhusu dhana na umuhimu wa kujiunga na bima ya Afya kwa Wote” amesisitiza Prof. Makubi.

Previous articleTANZANIA YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKA UINGEREZA
Next articleRAIS SAMIA SULUHU AFUNGUA SKULI YA MSINGI YA MWANAKWEREKWE ILIYOJENGWA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA FEDHA ZA UVIKO 19
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here