Home LOCAL TANZANIA YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKA UINGEREZA

TANZANIA YAPOKEA VIFAA VYA KUJIKINGA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KUTOKA UINGEREZA

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko kwa ajili ya watumishi wanaotoa huduma za afya na wateja wanaowahudumia,kutoka serikali ya Uingereza.

Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika Bohari ya Dawa (MSD) Keko Dar es Salaam,ambapo Mganga Mkuu wa serikali Prof. Tumaini Nagu amepokea vifaa hivyo kwa niaba ya serikali kutoka kwa Mkurugenzi wa Maendeleo wa ubalozi wa Uingereza nchini Tanzania, Kemi Williams.

Akipokea msaada huo Prof. Nagu ameishukuru Serikali ya Uingereza kwa vifaa hivyo na kueleza kuwa vifaa vya kujikinga na magonjwa ya mlipuko ni muhimu ili kupunguza hatari ya watoa huduma kuambukizwa wanapotekeleza majukumu yao.

Vifaa hivyo vitasambazwa na MSD kama Wizara ilivyoelekeza.

Previous articleMAKAMU WA RAIS AFUNGUA SKULI YA KWALE PEMBA
Next articleWANANCHI WAPATE ELIMU YA KUTOSHA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE – PROF. MAKUBI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here