Home SPORTS SIMBA SC YAMTAMBULISHA ROBERTINHO KUWA KOCHA MKUU

SIMBA SC YAMTAMBULISHA ROBERTINHO KUWA KOCHA MKUU

Timu ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC imemtangaza Kocha wa zamani wa Vipers SC ya Uganda Roberto Oliveira maarufu (Robertinho) kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili.

Akizungumza leo Disemba 3,2023 Jijini Dar es Salaam wakati wa utambulisho huo, Mwenyekiti wa Simba SC Murtaza Mangungu amesema kuwa wamemchukua Kocha Robertinho wakiamini uzoefu wake katika kufundisha soka, na kwamba wanaamini kufikia malengo yao pamoja na kufika mbali zaidi katika mashindano mbalimbali.

“Kocha Robertinho ana uzoefu mkubwa katika kufundisha soka, na sisi tumeamini uzoefu wake na tunaamini atatufikisha kwenye malengo yetu ambayo tumeyaweka kama Klabu,” amesema Mangungu.

Kwa upande wake Kocha Robertinho amesema kuwa  amekuja Simba SC kufanikisha malengo ya Klabu hiyo ambayo ni pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) msimu wa 2022-2023.

“Wakati nikiwa Vipers SC, mipango mizuri na malengo ni vitu ambavyo vilitufikisha kwenye malengo yetu ya kuwatupa nje ya Mashindano Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo tena kwenye uwanja wao na sisi kutinga makundi,” amesema Robertinho 

Previous articleKATIBU MKUU WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA OFISI YA WMA DODOMA
Next articleSIMBA SC YAPOKEA KICHAPO CHA 1-0 NA MLANDEGE FC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here