Home BUSINESS KATIBU MKUU WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA...

KATIBU MKUU WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA OFISI YA WMA DODOMA

Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Wakala wa Vipimo Makao Makuu Dodoma ili kujiridhisha na kasi na utendaji kazi katika mradi huo.

Dkt. Hashil ameipongeza WMA kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa Ofisi ya Makao Makuu na pia ameupongeza uongozi kwa jinsi wanavyoendeleza ujenzi wa Ofisi za Mikoa kwa lengo la kuboresha mazingira mazuri ya utendaji kazi.

Amesema kuwa ujenzi wa Ofisi ni muhimu sana na ujenzi wake unatumia fedha za Serikali ambazo ni fedha za walipa Kodi hivyo tunatakiwa tuzisimamie sana na tuhakikishe kila kitu kinachopaswa kufanyika kinafanyika ndani ya muda wake.

Amempongeza Mkandarasi kwa spidi nzuri ya ujenzi na amesema ni matumaini yake ujenzi utawahi kukamilika kabla ya muda waliojiwekea. Kadharika amemtaka Mkandarasi kuhakikisha manunuzi ya vifaa yanafanyika mapema ili kuondoa vikwazo vya ujenzi kuchelewa.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Bi. Stella Kahwa amemshukuru Katibu Mkuu Dkt. Hashil Abdallah kwa kutembelea ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu na kuhaidi kufanyia kazi maelekezo aliyotoa ili mradi uweze kukamilika kwa wakati.

Pamoja na hayo, Bi. Stella ameeleza kuwa ujenzi huu ulianza July 2022 na mpaka sasa kazi imefanyika kwa asilimia 38 hivyo kwa Kasi hiyo anaamini ujenzi utakamilika mapema kabla ya muda ila kwa ubora wa hali ya juu.

Ameeleza kuwa Jengo hilo litakuwa na Ofisi ya Makao Makuu lakini pia zitakuwepo Ofisi za Mkoa wa Dodoma. Vilevile, kutakuwa na maabara ya kisasa pamoja na mitambo ya kupima Mita za Umeme pamoja na Dira za Maji.

Imeandaliwa na Sehemu ya Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma

      

Previous articleRAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKITANGAZA KUHUSU KUFANYIKA KWA MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
Next articleSIMBA SC YAMTAMBULISHA ROBERTINHO KUWA KOCHA MKUU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here