Home LOCAL RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI LEO JANUARI 05 – ...

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI LEO JANUARI 05 –  2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan,  amemteua Dkt. Ellen Mkondya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa – Muhimbili. Dkt. Mkondya ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

(2) Amemteua Bw. Justine Peter Mwandu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Bima la Taifa (NIC). Bw. Mwandu ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania Reinsurance (TANRE).

(3) Amemteua Prof. Verdiana Grace Masanja kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI). Masanja ni Profesa wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.

(4) Amemteua Bw. Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania. Bw. Mwakapeje alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Huduma za Kisheria kwa Umma, Wizara ya Katiba na Sheria. Bw. Mwakapeje anachukua nafasi ya Bw. Casmir S. Kyuki ambaye atamaliza kipindi chake tarehe 07 Januari, 2023.

(5) Amemteua Bi. Fatma Mohamed Abdallah kuwa Mkurugenzi

Mwendeshaji wa Puma Energy Tanzania. Bi. Abdallah ni Meneja wa Kampuni ya Puma Energy nchini Geneva. Aidha, Bi. Abdallah anachukua nafasi ya Dominic Dhanah ambaye amemaliza muda wake.

(6) Amemteua BW. David Zacharia Kafulila kuwa Kamishna wa Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP). BW. Kafulila ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mstaafu.

Teuzi hizi zinaanza mara moja.

Zuhura Yunus,

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.

Previous articleTEF: MWAKA 2023 NI WA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA HABARI NCHINI
Next articleMAGAZETI YA LEO IJUMAA JANUARI 6 – 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here